KIUNGO wa Mbeya city fc ,
Ramadhani Chombo ‘Rendondo’ ameionya
timu ya Yanga ya jijini Dar Es
Salaam kuwa ijiandae vya
kutosha itakapokuja jijini hapa
mwanzoni mwa juma lijalo kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara kati ya timu hizo mbili uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mei 10
mwaka huu.
Akizungumza na mbeyacityfc.com
mapema leo, Redondo aliyekosa michezo
miwili ya awali kupisha majeraha ya mguu kabla ya kurejea na kuichezea City
kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar aliweka wazi kuwa ana imani kubwa na kikosi
cha sasa cha timu yake, hasa baada ya ujio
kocha Kinnah Phiri aliyefanikiwa kuyaondosha ‘makandokando’ yote
yaliyokuwa nasababisha timu kufanya vibaya kwenye michezo iliyopita.
“Nadhani Yanga wanatakiwa
wajiandae vizuri, wanakuja kukutana na
kikosi cha City ambacho kiko kwenye wakati mzuri
hivi sasa,hivyo wasitegemee mteremko,ujio wa kocha Phiri
umeiimarisha zaidi timu yetu, ametupa muongozo mzuri na amefanya kazi
kubwa kuweka timu sawa, hivyo hao
wanaokuja wajue watakutana na upinzani mkali,timu yetu sasa inacheza tofauti sana na ilivyokuwa
inacheza hapo mwanzo”, alisema.
Akiendelea zaidi Redondo, aliyewahi kucheza kwa mafaniko
kwenye timu za Ashanti, Simba na Azam Fc
alisema kuwa anafahamu mchezo huu utakuwa
mgumu pande zote kwa sababu kila timu
inahitaji matokeo kulingana na hali
ilivyo kwenye msimamo, Yanga
ikitaka kujihakikishia ubingwa na
City ikihitaji kujiweaka kwenye mazingira mazuri zaidi licha ya kuwepo kwa uhakika
kuwa itasalia kwenye ligi.
Kuhusu majaaliwa yake kwenye
kikosi cha City Redondo alisema kuwa
anaimani kubwa atakuwa sehemu ya
kikosi msimu ujao, na kuweka wazi furaha yake
ya kuwa mchezaji wa timu hii
tangu alipojounga nayo mapema mwezi
Januari.
“Nilijiunga na City mapema
mwezi januari, nakumbuka ilikuwa ni
wakati wa usajiri wa dirisha dogo,
binafsi nina furaha hapa na
nitaka kufanya kazi zaidi na kwa uwezo wangu wote kwa sababu lengo langu ni kuendelea kuwepo, kwangu
mimi hii ni timu nzuri kuliko zote nilizowahi kucheza, kuna wakati
najiuliza kwa nini sikuwa huku mapema
lakini hii ni soka na maisha ya
mchezo huu ndiyo yalivyo” alimaliza
0 comments:
Post a Comment