Katibu mkuu wa TUICO Boniface Nkakatisi (kushoto)
akisaini mkataba wa hiari wa hali bora na maslahi ya wafanyakazi na Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group Roberto Jarrin (kulia) jana mjini
Dodoma katikati anayeshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu
sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira,na Watu wenye ulemavu Mh.Jenista Mhagama
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group Roberto
Jarrin (kulia) akikabidhiana mkataba wa hiari wa hali
bora na maslahi ya wafanyakazi na Katibu Mkuu wa TUICO Boniface
Nkakatisi (kushoto) jana mjini Dodoma mara baada ya kutiliana saini mjini
Dodoma, katikati anayeshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
mkuu sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira,na Watu wenye ulemavu, Mh.Jenista Mhagama
Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya TBL
Group wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira,na Watu wenye ulemavu ,Jenista Mhagama
baada ya kusaini rasmi mkataba wa hiari wa hali bora na maslahi ya wafanyakazi
kati ya kampuni hiyo na TUICO
Meneja Masoko na Udhamini kampuni ya TBL
Group, George Kavishe (kushoto) akimwonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri mkuu sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira,na Watu wenye ulemavu Jenista Mhagama
bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo alipotembelea banda hilo jana kabla ya
kusaini kwa mkataba wa hiari kati ya TBL na TUICO katika hoteli ya St Gaspar
Mjini Dodoma jana. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu
sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira,na Watu wenye ulemavu Jenista Mhagama akiangalia
moja ya bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo
Mtaalamu wa ubora kampuni ya bia TBL
Rebecca Semoka akimwonyesha zao la shayiri ambalo linatumika kutengenezea bia
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira,na Watu wenye
ulemavu Jenista Mhagama (kushoto )
*********************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
sera,bunge,kazi,vijana,ajira Watu wenye ulemavu Jenista Mhagama amesema kuwa
njia pekee ya kuleta ufanisi sehemu za kazi na kuondoa migogoro ni kuwepo na
uhusiano mzuri baina ya waajiri na wafanyakazi wao.
Akihutubia Uongozi na wafanyakazi wa TBL Group
wakati wa hafla ya kampuni hiyo kusaini mkataba na Chama Cha kutetea maslahi ya wafanyakazi
cha TUICO unaohusiana na maslahi bora ya wafanyakazi iliyofanyika jana katika
ukumbi wa Mt.Gaspar Mjini Dodoma,Waziri Mhagama alisema hakuna mafanikio
yanayoweza kupatikana katika mazingira yenye uhusiano mbaya baina ya
mwajiri na wafanyakazi wake. katika sehemu za kazi.
“Nawapongeza waajiri wanaokaa na wafanyakazi wao
na kukubaliana kuhusiana na masuala ya maslahi kama ambavyo TBL mnafanya na
waajiri wote wanapaswa kuzingatia suala hili ili kuleta tija na ufanisi sehemu
zao kazi ili kuongeza uzalishaji na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa”.Alisema Mhagama.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBL
Group,Roberto Jarrin alisema kuwa mtazamo wa kampuni hiyo ni kuwa kioo na mfano
wa uwekezaji mzuri nchini na mbali na kuongeza ubora na uzalishaji kwenye
bidhaa zake imejikita pia katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi wake,kuongeza
ajira nchini,kuwezesha vikundi vya wafanyabiashara wadogo na wa kati,kuchangia
pato la serikali kwa njia ya kodi.
Alisema TBL itaendelea kuunga mkono jitihada za
serikali kuleta maendeleo kwa kushiriki kusaidia miradi mbalimbali ya kuinua
maisha ya wananchi huusani wakulima na kuchangia pato la serikali kwa njia ya
kodi “Tunayo mikakati ya kuboresha maisha ya wakulima nchini
ambayo tayari tumeanza kuitekeleza ikiwemo kulipa kodi ambako tumekuwa
tukiongoza kulipa kodi na kutunukiwa tuzo mbalimbali”.Alisema.
Katibu mkuu wa TUICO Taifa, Boniface
Nkakatisi alipongeza hatua ya TBL kutiliana saini ya makubaliano ya ubora
wa maslahi na wafanyakazi wake kwa kuwa italeta ufanisi na kuondoa migogoro na
malalamiko “Mara nyingi chama chetu kimekuwa kikishughulikia
migogoro baina ya wafanyakazi na waajiri wao ,tukio kama hili la leo
linafurahisha na viwanda na makampuni yote yanapaswa kutekeleza
jambo hili”.Alisema.
Kabla ya kushuhudia utiwaji saini makubaliano
haya,Waziri Mhagama alitembelea maonyesho ya kampuni yaTBL Group na
kupatiwa maelezo kuhusiana na jinsi inavyoendesha shughuli zake na maelezo ya
bidhaa ambazo inazalisha.
0 comments:
Post a Comment