Mkuu wa mkoa
wa Mwanza John Mongella, amesema mkoa wa Mwanza unategemea kupokea Tani 500 za
Sukari zitakazo ingia katika mkoa huu zikitokea kiwanda cha sukari cha Kagera
Sugar tarehe 24, Mei, 2016, ambazo zinaingizwa mkoani hapo na muagizaji na
Msambazaji P.H Shah.
Hata hivyo
mkuu wa mkoa ameonya watu watakao uza sukari hiyo kinyume na bei elekezi kuchukuliwa
hatua za kisheria ikiwa nipamoja nakufikishwa katika vyombo vya dola.
Mongella
amesema pia kwamba, kupitia kamati yakushughulikia sukari, tayari wametoa
maelekezo kwa Wakuu wa wilaya jinsi yakushughulikia suala la sukari na kwamba
wasambazaji wote katika Wilaya lazima wazingatie maelekezo bila kuvunja
utaratibu utakao wekwa.
Mahitaji ya
sukari katika mkoa wa Mwanza ni Tani 1,500 kwa wiki kwa matumizi ya kawaida kwa
wananchi wake, hivyo kuwasili kwa tani 500 ukweli kwamba itasaidia kupunguza
uhaba wa sukari unao ukabili mkoa huu kwa sasa.
Hata hivyo
mkuu wa mkoa amewatoa wanachi hofu juu ya sukari kwakusema, tayari viwanda vya
hapa nchini vimekwisha anza uzalishaji wa sukari na kwamba muda si mrefu tatizo
la sukari litapungua kama sio kuisha kabisa.
Imetolewa na
Atley J. Kuni
Afisa habari na
Mahusiano, Ofisi ya mkuu wa Mkoa
MWANZA
24, Meil 2016
0 comments:
Post a Comment