Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala.
Na. Aron Msigwa - Dodoma.
Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 8
kuboresha miundombinu ya vyuo vya Afya kote nchini katika mwaka wa fedha
2016/2017 ili kuwawezesha wanafunzi wa fani ya Afya kusoma katika mazingira mazuri.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati
akijibu swali la Mbunge wa Muhambwe Mhe.Atashasta Justus Ntitiye, alieyata
kujua mkakati wa Serikali wa kuboresha vyuo vya Afya nchini hususan chuo cha
Uuguzi wilayani Kibondo kilicho katika jimboni lake. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Dkt.Kigwangala amesema Serikali katika mwaka wa fedha
2016/2017 imejipanga kuboresha mazingira ya vyuo vya Afya katika maeneo
mbalimbali nchini kikiwemo Chuo cha Uuguzi Kibondo ambacho kimetengewa shilingi
milioni 680.
Aidha, ameeleza kuwa vyuo vya Afya vimekuwa
vikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo madeni ya wazabuni wa vyakula
waliokuwa wakiidai Serikali kiasi cha shilingi Bilioni 6.8 kuanzia mwaka
2009 hadi 2015.
Amebainisha kuwa tayari Serikali imekwishahakiki madeni
yote ya wazabuni ili yaweze
kulipwa katika mwaka wa fedha 2016/2017
na kuongeza kuwa suala la usambazaji wa vyakula limeachwa chini Sekta binafsi
ili zifanye kazi hiyo.
Katika hatua nyingine Dkt.Kigwangala amesema Serikali
inaendelea kuangalia uwezekano wa kuyatumia majengo yaliyoachwa kwenye kambi za
wakimbizi zilizofungwa mkoani Kigoma hususan wilayani Kibondo ili yaweze
kutumika kama vyuo vya kutolea elimu ya Afya.
" Niko tayari nikishirikiana na waheshimiwa
wabunge kwenda mkoani Kigoma kuzungumza na viongozi wa mkoa huo ili tuweke
utaratibu wa namna ya kuyatumia majengo hayo" Amesisitiza Dkt.Kigwangala.
0 comments:
Post a Comment