ZOEZI kusaka nyota wapya
(vijana) ambao wataingizwa kwenye timu
mbili za Mbeya City Fc U20 na ile ya wakubwa limefikia kwenye hatua nzuri
hivi sasa baada ya wachezaji 44 kupatikana kwenye mchujo wa awali uliolifanyika
leo ikiwa ni baada ya siku nne za mazoezi.
Akizungumza na
mbeyacityfc.com, mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya leo (Clinic day 5)
kwenye uwanja wa Sokoine kocha msaidizi wa City, Mohamed Kijuso amesema kuwa
Vijana 44 wamefanikiwa kuvuka kwenye
mchujo wa kwanza hivyo wataingia kwenye
wamu ya pili inayotaraji kuanza hapo kesho kwenye uwanja wa Sokoine.
“Tulikuwa na kundi kubwa la
wachezaji zaidi ya 106, baada ya mchujo leo, tumefanikiwa kupata 44 ambao wataingia kwenye awamu ya pili hapo
kesho, lengo letu ni kuona tunapata
Cream nzuri kwa ajili ya timu yetu ya vijana na pia wachezaji saba ambao watakuwa tayari kucheza
kwenye timu kubwa msimu ujao”, alisema.
Kuhusu lini itakuwa siku ya
mwisho, kocha huyo kijana alitanabaisha kuwa, mchakato huu wa kuska vipaji
ulikuwa ufikie tamati hapo kesho lakini uongozi wa City umeamua kusogeza mbele
mpaka siku ya jumamosi ambapo wachezaji
watakaopatikana kwenye mchujo wa kesho
watapata nafasi ya kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na timu ya Ilemi Fc.
“Ilikuwa tuhitimishe kesho
lakini tumesogeza mpaka jumamosi ambapo vijana wetu wapya watakaopatikana
watacheza mchezo wa kirafiki , na baada ya hapo zoezi litafungwa tayari wa kusubiri
maandalizi ya msimu mapema mwezi ujao” alimaliza.
0 comments:
Post a Comment