Meneja wa kuendeleza vipaji wa TBL Group
,Lilian Makau akitoa mada wakati wa semina semina ya kuwaandaa wanafunzi wanaosoma
vyuo vikuu kuingia kwenye ajira watakapomalizika masomo
yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
*************
Taasisi na makampuni mbalimbali mwishoni mwa wiki yalishiriki katika semina ya kuwaandaa wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu kuingia kwenye ajira watakapomalizika masomo yao ambayo ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kushirikisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya juu.
Kampuni ya
TBL Group ilishiriki katika semina hiyo ambapo Meneja wake wa kuendeleza vipaji Lilian
Makau,alitoa mada kuhusiana na jinsi ya kuhimili kufanya kazi kwenye
kampuni kubwa na zenye mifumo thabiti ya kiutendaji na
changamoto za kupata ajira.
Wanafunzi
wengi pia walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu taratibu za ajira
katika kampuni ya TBL ambapo aliwaeleza kuwa kampuni inatoa fursa za ajira kwa
watanzania wote na taratibu zake za ajira ziko wazi na pia kuwa imekuwa na
utaratibu wa kuajiri wasomi waliohitimu mafunzo vyuoni na kuwapatia mafunzo ya
ndani na wengi wao wametokea kuwa na utaalamu wa kiwango cha juu baada ya muda
mfupi kwenye ajira zao.
Wanafunzi wakisikiliza mada na kuuliza maswali
Meneja wa kuendeleza vipaji wa TBL Group
,Lilian Makau akitoa mada wakati wa semina semina ya kuwaandaa wanafunzi wanaosoma
vyuo vikuu kuingia kwenye ajira watakapomalizika masomo
yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam
wakichukua anuani ya mtoa mada
Baadhi ya wanafunzi wakipata maelekezo kutoka
kwa Meneja wa Kuendeleza vipaji wa TBL Group,Lilian Makau muda mfupi baada ya
kumalizika semina
0 comments:
Post a Comment