Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gelasius Gaspar
Byakanwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.
Taarifa
iliyotolewa leo Ikulu Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 08 April, 2016.
Bw. Byakanwa
anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Antony Mtaka aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu.
Kabla ya Uteuzi
huo, Bw. Byakanwa alikuwa Katibu wa Rais Msaidizi Mwandamizi.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
08 Aprili,
2016
0 comments:
Post a Comment