Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akitoa ufafanuzi wa masuala ya mikataba ya
ajira wakati wa mkutano na Kamati ya Kudumu ya Waziri Mkuu ya Kutatua kero na changamoto katika sekta ya usafiri wa barabara katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 1, 2016.
Wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Waziri Mkuu ya Kutatua kero na changamoto katika sekta ya
usafiri wa barabara wakifuatilia hoja za Naibu Waziri Uchukuzi Mhe.
Edwin Ngonyani (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kamati hiyo tarehe
1.4.2016 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (DARCOBOA),Sabri Mabrouk
akitoa hoja ya uboreshwaji wa mikataba ya madereva wakati wa mkutano wa
Kamati ya Kudumu
ya Waziri Mkuu ya Kutatua kero na changamoto katika sekta ya usafiri wa
barabara uliofanyika tarehe 1.4.2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi
ya Waziri Mkuu.
\Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akititoa ufafanuzu wa kisheria wakati wa mkutano wa Kamati ya Kudumu
ya Waziri Mkuu ya Kutatua kero na changamoto katika sekta ya usafiri wa
barabara uliofanyika 1.4.2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya
Waziri Mkuu.(Picha Zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
*****************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ameiagiza kamati ya Kudumu ya Waziri Mkuu ya
Kutatua kero na changamoto katika sekta ya usafiri wa barabara kuangalia upya
mikataba ya madereva ili kuhakikisha haki za madereva zinalindwa.
Mhe mhagama alitoa agizo hilo wakati wa mkutano wake na Kamati hiyo uliofanyika
Aprili 1, 2016 katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es
Salaam kwa lengo la kuangalia namna bora ya kukabiliana na changamoto
zinazoikabili sekta ya usafirishaji.
Katika kikao cha Kamati hiyo inayoundwa na Wamiliki wa malori, daladala,
mabasi, vyama vya abiria, Idara ya Usafirishaji, Shirika la viwango, Wakala wa
Vipimo, Jeshi la polisi, watu wa usalama barabarani, TANROADS na Umoja wa
Wasafirishaji Abiria Dar es Salaam (UWADAR) mhe. Mhagama alisisitiza kuwa
Serikali haitawafumbia macho wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao hawazingatii
mikataba ya kazi kwa madereva.
“Ninaagiza mikataba ya maderva iangaliwe upya na ikiwezekana yaainishwe majina
ya wamiliki wa magari wanaokiuka haki na sheria zilizopo za kuwapa madereva
mikataba na stahiki zao ili sheria iweze kuchukua mkondo wake,”alisema Mhagama
Kutokana na changamoto mbalimbali za madereva zilizobainishwa
wakati wa mkutano huo Mhe.Waziri aliwataka wajumbe wote kuangalia namna
nzuri ya kukabili changamoto hizo ili kuhakikisha malalamiko ya madeva yanaisha
na kufanya sekta hiyo kuwa na amani na
utulivu.
“Lengo kuu ni kuona sekta ya usafirishaji inakuwa salama na yenye amani kwani
ikumbukwe sekta hii ni nyeti, inabeba roho za watu wengi kila iitwapo leo kwa
kuwasafirisha mikoani na nje ya mikoa.” Alisisitiza Mhagama.
Nae mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Leonard Chamuliho aliomba kamati kuyafikia
maazimio ya muhimu yaliyojadiliwa na huku akisisitiza agizo la mhe. Mhagama la
kuwataka wamiliki na waajiri wote kuzifuata na kuzitekeleza sheria za mikataba
kwa waajiriwa wote.
0 comments:
Post a Comment