Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akikabidhi koti maalum la usalama barabarani Bw. Thobias Msua mmoja wa waendesha Bodaboda wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 4 na wametoa msaada huo kwa waendesha bodaboda zaidi ya 4000, makabidhiano hayo yamefanyika Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam.
KAMPUNI ya Ulinzi ya SGA imetoa
msaada wa vifaa kusaidia waendesha bodaboda Mtaa Mbezi A, katika kujiepusha na ajali
katika siku ya usalama duniani.
Akizungumza wakati wa kakabidhi vifaa
hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Erick Sambu amesema kuwa vifaa
walivyopewa vitasaidia katika kujiepusha na ajali kutokana na dereva wa gari
kuona kifaa hicho.
Amesema kuwa vifaa hivyo vina thamani
ya sh.milioni Nne na kuahidi kuendelea kutoa msaada katika makundi mbalimbali
kutokana na kazi yao ya kuangalia usalama.
Sambu amesema kuwa SGA katika kuadhimisha siku ya usalama duniani na
kuwataka wadau wengine kuunga mkono katika kuwangalia watu bodaboda.
Naye Mwakilishi wa Mwanyekiti wa
Serikali ya Mtaa Mbezi A, Carolyne Ngoda amesema kuwa SGA wameokoa maisha ya
vijana wao wanaoshughuli na biashara ya kusafirisa watu kutoka sehemu moja
kwenda nyingine.
0 comments:
Post a Comment