INAWEZEKANA kuwa soko na eneo la viwanda vidogo la Vetenari lililopo kando ya barabara kuu ya Mandela, Wilaya ya temeke jijini Dar es Salaam hawana vyoo. Na kama vipo basi havitumiki ipasavyo kiasi cha kuwafanya watu waliopo katika eneo hilo kutumia uwanja wa mpira katika soko hilo kama sehemu ya kujisaidia haja ndogo. Camwera ya Father Kidevu iliwanasa vijana wawili wakielekea kutimiza haja yao hiyo uwanjani hapo na katika madimbwi ya maji jirani na watu waliokuwa wakishughulika na kazi zao.
Tayari kijana wa kwanza amefika katika maliwato yake yasiyo rasmi na anaanza kujiandaa huku mwenzake akifuata.
Vijana hao wakichafua mazingira kwa kukojoa hovyo.
Ni vyema mamlaka husika zikafika katika eneo hilo na kuwapa elimu ya utumiaji vyoo ili kuwaepusha watu wa sokoni hapo kujiepusha na magonjwa ya mlipuko kwani wakati mwingine maji hayo yaliyotuama jirani na wanapokojoa huyatumia kwa kunawa.
0 comments:
Post a Comment