Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata utepe kuzindua magari ambayo yametolewa na Mfuko wa GSM kwaajili ya
kusidia kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa pamoja na
watoto wenye migongo wazi katika kambi itakayofanyika katika mikoa ya Mwanza
Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka
Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa
kambi ya upasuaji ya watoto wa wenye vichwa vikubwa na watoto wenye
matatizo ya mgongo wazi ambapo Mfuko wa GMS kushirikiana na Taasisi ya
Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili wataanza kambi hiyo
katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka
4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15
mpaka 17. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba
na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma na Mkurugenzi wa tiba MOI
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Samwel Swai.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili,
Othman Kiloloma katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam leo kuhusiana na kambi ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa
vikubwa na watoto wenye Migongo wazi. Kulia ni kuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Afisa
Uhusiano wa Mfuko wa GSM, Khalfan Kiwamba akizumgumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na GSM kutoa mchango wake kwa
kusaidia watoto wenye matatizo ya Mgongo wazi na watoto wenye vichwa
vikubwa. Kusoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimpa ufunguo za magari,Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma leo jijini Dar es Salaam.
*******************
Kambi itakayofanyika katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17.
Upasuaji huo utakaofanyika chini ya madaktari hao bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, iliyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili, inatarajiwa kuwafikia watu 800 mpaka 1000 na baadaye kuwafanyia upasuaji watoto 80 hadi 100 nchi nzima.
Upasuaji huo utakaofanyika chini ya madaktari hao bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, iliyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili, inatarajiwa kuwafikia watu 800 mpaka 1000 na baadaye kuwafanyia upasuaji watoto 80 hadi 100 nchi nzima.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi
msaada huo, Makonda amepongeza MOI kwa kutafuta mbinu za kuendeleza
sekta ya afya nje ya bajeti ya serikali.
Kampuni ya GSM itagharamia ziara hiyo, ambapo mpaka jana ilikabidhi pia magari matatu yatakayotumika katika ziara hiyo.
0 comments:
Post a Comment