Nafasi Ya Matangazo

March 08, 2016

Waziri wa Afya,Maendeleo Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Biafra  jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dk.Hamis Kigwangalla akitoa maelezo ya ushiriki wa Mbunge wa Njombe Kusini, Edward Mwalongo kwa kupaza sauti katika bunge juu ya  mtoto wa kike kupewa dhana  ya kujikinga wakati wa hedhi ili aweze kusoma katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya  Biafra jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimkabidhi tuzo Mbunge wa Njombe Kusini, Edward Mwalongo kwa kwa kupaza sauti katika bunge juu ya  mtoto wa kike kupewa dhana  ya kujikinga wakati wa hedhi ili aweze kusoma katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya  Biafra jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  akimkabidhi hundi ya sh.milioni tano, Dereva wa Bodaboda, Sikudhani Daudi zilizotolewa na Benki ya DCB ikiwa na lengo ya kukuza biashara katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya  Biafra jijini Dar es Salaam.  
Wanawake kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper (TSN) Limited na Standard Printer wachapishaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News, Habari Leo na Habarileo Jumapili pamoja na gazeti la Spoti Leo wakishiriki katika maandamano ya siku ya wanawake iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. 
Wanawake kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper (TSN) Limited na Standard Printer wachapishaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News, Habari Leo na Habarileo Jumapili pamoja na gazeti la Spoti Leo wakishiriki katika maandamano ya siku ya wanawake iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. 

Wanawake kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper (TSN) Limited na Standard Printer wachapishaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News, Habari Leo na Habarileo Jumapili pamoja na gazeti la Spoti Leo wakishiriki katika maandamano ya siku ya wanawake iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. 
Wanawake kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper (TSN) Limited na Standard Printer wachapishaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News, Habari Leo na Habarileo Jumapili pamoja na gazeti la Spoti Leo wakishiriki katika maandamano ya siku ya wanawake iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. KUONA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Wanawake katika vikundi vilivyopata mkopo katoka kwa benki ya DCB wakiwa katika picha ya pamoja na hundi zao leo katika siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja Biafra leo.
Wanawake wa Mamlaka wa Chakula na Dawa (TFDA) wakiwa na bango  katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya  Biafra jijini Dar es Salaam.
Wanawake wakiwa wameketi wakimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (hayupo pichani) katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya  Biafra jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya Jamii).  
***************
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
BENKI ya Wanawake Nchini(TWB)imekuwa jipu kutokana na kutokuwa na msaada wa kuwaendeleza wanawake ili waweze kunyanyuka kiuchumi.

Hayo ameyasema leo Waziri wa Afya,Maendeleo Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati kilele cha siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila Machi 8 katika mwaka,amesema kuwa benki ya TWB haijatengeneza mazingira rafiki kwa wanawake ili waweze kuitumia.

Amesema kuwa benki zingine zimeweza kufanya kazi za kuwainua wanawake kwa kuwapa mikopo lakini benki ya TWB haifanyi hivyo huku wakijua na wajibu wa kufanya hivyo.

Ummy amesema licha ya changa oto ya mikopo kuna baadhi ya Halmashauri hazitoi asilimia tano katika mfuko wa wanawake katika kuwaendeleza kiuchumi.

Ummy amesema wanawake wanatakiwa kufika asilimia 50 katiki kuweza kwenda sambamba na wanawake lazma waonyeshe uwezo na fursa mbalimbali za uchumi kuzitumia.

Amesema wanawake wakipata nafasi ni sawa na kuwa na jamii nzima yenye mafanikio ya mwanamke mmoja hivyo kila mwanamke afanye kazi kwa kujituma katika nafasi yake iwe ya kiuchumi ,kutoa huduma kwa jamii.

Aidha amesema kuwa kila wanawake 10 ,wanawake sita (6) wanamaambukizi  vya virusi ukimwi na kila wanaume 10 wanne (4) wanaambukizi ya virusi vya ukimwi.

Waziri wa Afya amesema kutokana na takwimu hizo lazima licha ya kuwakamata wanawake wanaojiuza ‘makahaba’ kunahitaji na kuwakamata wanaume ambao wanafanya mchezo huo katika kupunguza maambukizi kwa wanawake.

Katika Maadhimisho hayo mbunge wa Njombe Kusini, Edward Mwalongo amepata tuzo kupaza sauti katika bunge juu ya  mtoto wa kike kupewa dhana  ya kujikinga wakati wa hedhi ili aweze kusoma.

Waziri Ummy ameipongeza Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kuendelea kuelimisha wanawake juu ya vipodozi feki pamoja na vyakula  kutokana na kutambua wajibu kulinda wanawake.
Posted by MROKI On Tuesday, March 08, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo