Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiongea na Menejimenti ya Wakala wa
Majengo Tanzania - TBA (hawapo pichani) wakati alipotembelea Ofisi za Wakala
huo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiongea na Wafanyakazi wa Wakala wa
Majengo Tanzania –TBA kutoka mkoa wa Pwani na Dar es salaam katika mkutano wa Wakala huo uliofanyika Karimjee jijini Dar
es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga
(kulia), akiongea na wafanyakazi wa TBA kutoka mkoa wa Pwani na Dar es salaam
katika mkutano wa Wakala huo uliofanyika jijini Dar es salaam. Katikati ni
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifuatilia.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga (kushoto), akizungumza na
wafanyakazi wa Wakala huo (hawapo pichani) kwenye mkutano wa wafanyakazi wa
Wakala huo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Huku Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
(Sekta ya ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga wakisikiliza.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga (kulia), akifafanua jambo kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya
Waziri huyo kukagua mradi wa jengo la ghorofa saba eneo la Sida Eda Estate
jijini Dar es salaam. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
*********************
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)
kuzingatia thamani ya fedha kwa kila mradi wa ujenzi wa nyumba wanaoutekeleza
nchini.
Ametoa agizo hilo wakati
akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa saba katika eneo la Sida Ada
Estate linalojegwa na Wakala huo jijini Dar es Salaam.
Amemuagiza Mtendaji Mkuu wa
TBA Arch.Elius Mwakalinga kuhakikisha kuwa wapangaji wote wanaoishi kwenye
nyumba za Wakala huo kulipa kodi zote kwa wakati na watakaoshindwa wahame mara
moja.
“Natoa mwezi mmoja kwa
watumishi ambao hawajalipa watafute sehemu nyingine ya kukaa, ili wakala
apangishe nyumba hizo kwa anaeweza kulipa kwa wakati “,amesema Profesa Mbarawa.
Amewataka watumishi wote wa
TBA kufanya kazi kwa malengo yanayopimika ili kuweza kuleta tija na kuongeza
pato la Wakala.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu
wa TBA Arch.Elius Mwakalinga amemhakikishia Waziri kuwa Wakala unaendelea kutoa
huduma ya matengenzo na ujenzi wa nyumba na ofisi za Serikali katika mikoa yote
25 ya Tanzania Bara.
Aidha, ametaja baadhi ya
changamoto zinazokabili Wakala huo ni mahitaji makubwa ya nyumba kwa watumishi
wa umma kuliko uwezo wa Wakala ambapo kwa sasa mahitaji ya nyumba za watumishi
wa Umma ni takribani laki nne.
Ameongeza kuwa kasi ya
mabadiliko ya teknolojia hailingani na uwezo wa wakala hivyo ameomba Waziri
Profesa Mbarawa kuuwezesha Wakala huo kimtaji na kimafunzo ili uweze kushindana
na soko na kuboresha sekta ya ujenzi wa nyumba nchini.
Naye Katibu Mkuu wa Sekta ya
Ujenzi, Eng. Jospeh Nyamhanga amesisitiza umuhimu wa kubadili mtazamo wa Wakala
kufanyakazi kimazoea na badala yake kuwa na mtazamo wa kibiashara ili kuweza
kujitegemea kama lengo la kuanzishwa kwa wakala huo. Aidha ameongeza kuwa
atahakikisha kuwa Wakala huo unapata magari kwa kuongeza tija katika utendaji kazi.
Wakala wa majengo umetumia
kiasi cha takribani Bilioni 5 kwa ujenzi wa jengo la ghorofa saba lililojengwa
katika eneo la Sida Ada Estate ambapo ujenzi huo umekamilika kwa asilimia tisini
na tano.
0 comments:
Post a Comment