Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA Aisha Bade akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za shirika hilo zilizoko Ilala kuhusu kuadhiisha siku ya wanawake duniani pamoja na changamoto mbalimbali ambazo shirika hilo limepambana nazo katika kutetea haki za wanawake hapa nchini, kutoka kushoto ni Nasieku Kisambu Mkurugenzi wa Miradi TAWLA na kulia ni Amaria Marenji Mjumbe wa Kamati ya Uongozi TAWLA.
Baadhi ya wakuu wa vitengo na maofisa wa TAWLA wakiwa katika mkutano huo.
Tike Mwambipile Mkurugenzi wa TAWLA akielezea jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo
***********
Kwanza kabisa, hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema na fadhila, kwa kutujalia uhai na afya njema na kutuwezesha kujumuika hapa leo kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Awali ya yote napenda kuwashukuru waandishi wa habari kwa kutenga muda wenu na kuwa nasi mbali na kuwa na shughuli nyingi. Natambua vyombo vya habari ni njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa haraka, lakini pia nyenzo muhimu katika kuhamasisha na kutetea upatikanaji wa haki za wanawake na watoto nchini. KUSOMA AIDI BOFYA HAPA
Napenda pia kushukuru wanachama, uongozi wa TAWLA pamoja na wafanyakazi mliopo hapa.
Ndugu waandishi wa habari, Siku ya Wanawake ilianza kuadhimishwa mwanzoni mwa miaka ya 1900 kwa kupitia wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani walioandamana kupinga mazingira duni ya kazi zao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira. Kutokana na hali hiyo, nchi ya Marekani ilikubali kuwa na siku ya maadhimisho ya kitaifa ili kutafakari masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wa wanawake.
Baadaye Umoja wa Mataifa ulipaoanzishwa mwaka 1945 uliridhia siku ya tarehe 8 Machi iwe Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa ulitokana na kukubali kwake kwamba masuala ya haki, maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo maalumu na wa pekee. Tanzania ilianza kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka 1996, maadhimisho yamekuwa yakiandaliwa Kitaifa na katika ngazi ya mkoa.
Katika kuadhimisha siku ya wanawake leo tarehe 8 March, 2016, TAWLA imeona ni vyema kushirikiana na vyombo vya habari kwa lengo la kuikumbusha jamii juu ya umuhimu wa usawa wa kijinsia. Kauli mbiu ya mwaka huu 2016, ni 50-50 ifikapo 2030, Tuongeze jitihada (Planet 50-50 by 2030: Step It Up for Gender Equality). Kauli mbiu hii inalenga katika kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali za Kimataifa/ kikanda na kitaifa zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na wanawake katika kuhakikisha ushiriki wa wanawake kiuchumi, kijamii, na kisiasa unatambuliwa na kuheshimiwa na jamii kwa ujumla.
Ndugu waandishi, wanawake wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo has pale mazingira yanapowaruhusu. Ni kwa misingi hio basi, TAWLA inasisitiza kwamba kila Mtanzania anajukumu la kuweka mazingira ya usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana kushiriki katika masuala ya kiuchumi, elimu, ajira, siasa na sheria ifikapo mwaka 2030. Ni kutokana na misingi hio chama kinatoa ahadi zifuatazo.
TAWLA INAAHIDI:
- Kusaidia wanawake kufikia malengo
TAWLA inaahidi kudumisha uendelevu wa huduma za msaada wa kisheria kwa makundi maalumu. Hili linafanyika kwa wanachama kutumia taaluma yao ya sheria pamoja na sheria za nchi katika kuhakikisha haki inatendeka na hasa kusisitiza kutekelezwa kwa mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhiai. Katika hili tutaendelea kufanya ushawishi wa kurasimisha sheria zenye uwiano na usawa wa kijinsia.
- Kuondoa ubaguzi wa wazi na uliojificha.
TAWLA imegundua kwamba kuna changamoto kubwa katika ubaguzi na ukatili kwa wanawake na suala hili limekua ni tatizo hapa nchini. Ubaguzi na ukatili vimechangia sana katika kuwakwamisha wanawake kufikia ndoto na malengo yao. Ili kufanikisha hili Chama kinaahidi kuendelea kutoa elimu kwa jamii na kuendesha mikutano ya kubadili mitazamo kwa jamii dhidi ya wanawake.
- Wito kwa uongozi wa kijinsia na uwiano
Chama kinatambua uwezo wa mwanamke katika ngazi mbalimbali za uongozi kutoka kwenye kaya mpaka ngazi ya kitaifa. Ushiriki wa wanawake katika uongozi unawapa fursa ya kushiriki katika ngazi za maamuzi ambayo yanamanufaa kwa wanawake na wanaume kwenye jamii. Kwa misingi hio, chama kimeanzisha programu ya kuwakutanisha pamoja wanawake walioshika ngazi mbalimbali za uongozi nchini na ambao wanatarajia au ni wapya katika ngazi za uongozi kwa lengo la kuhakikisha kwamba wanakuwa viongozi wazuri, bora na wa kutegemewa lakini pia wenye kuleta mabadiliko katika jamii. Programu hii inalenga kuwashawishi wanawake mbalimbali kugombea ngazi za uongozi ili kuhakikisha kwamba masuala ya wanawake yanapewa kipaumbele.
- Kuthamini Usawa wa kijinsia kwa jamii.
Tutaendelea kuhamasisha jamaii kuhusu kuelewa kwamba usawa wa kijinsia sio suala la wanawake peke yao bali ni jukumu la kila mwanajamii na linahitaji ushirikiano kutoka kwa wanaume na wanawake pamoja na jamii kwa ujumla. “kwa kuongezea usawa wa kijinsia kutachangia kuboresha maisha ya wanawake na wasichana, familia, jamii na taifa kwa ujumla. Endapo vitendo vya ubaguzi wa kijinsia vitapigwa vita ina maana idadi ya watoto wa kike watakaokuwa wanaenda shule itaongezeka, familia zitakuwa na afya bora, uzalishaji katika kilimo utaongezeka na hivyo kipato kitaongezeka.
- Kujenga utamaduni chanya
TAWLA inatambua kwamba katika jamii zipo mila na desturi mbalimbali ambazo hutofautiana kutokana na mazingira. Aidha baadhi ya tamaduni hizo zimekuwa kikwazo kwa wanawake na wasichana kwa karne nyingi. Ili kujenga utamaduni chanya chama kimekua kikifanya uchechemuzi juu mabadiliko ya sheria kandamizi na kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kubadili mitazamo na tamaduni hasi ambazo ni kandamizi. Kwa kuisadia jamii kujenga mitazamo chanya Chama kimekuwa kikifanya mazungumzo na jamii katika mada mbalimbali kama vile madhara ya ndoa za utotoni, ukeketaji na ukatili wa kijinsia.
Chama katika kuadhimisha siku ya mwanamke dunia, itafanya shughuli zifuatazo;
- Itafanya mazungumzo na waandishi wa habari leo tarehe 8/3/2016.
- Kutoa msaada wa kisheria katika wilaya zote za Dar es salaam na katika ofisi zake za mikoani kwanzia tarehe 7/3/2016 mpaka 10/3/2016.
- Kufanya midahalo/ mazungumzo katika jamii.
- Kampeni ya kutumia mitandao ya kijamii kuhamasisha na kutoa elimu ya usawa wa kijinsia kwa mwezi mzima wa March.
Chama pia kitashirikiana na taasisi ya Wanawake wenye mafanikio (TWA), kwa kuhamasisha wanachama wake kushirikia katika shughuli zifuatazo;.
- Kushiriki katika matembezi ya kilomita sita ambayo yataanzia kwenye “Uwanja wa Mbio za Mbuzi”, Masaki, Dar es Salaam Jumamosi Machi 5, 2016
- Kushiriki katika Kongamano la Siku ya Kimataifa ya Wanawake litakaofanyika kwenye Hoteli ya Regency Kilimanjaro, Jumapili, Machi 6.2016.
Taarifa kwa wahariri:
TAWLA inatoa huduma zifuatazo
- Kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto, huduma hizo hutolewa Jumatatu na Jumatano kwa Dar es salaam na kila siku katika ofisi zetu mikoani – Tanga, Arusha, Dodoma, na Mwanza . Pia kupitia toll free number: 0800110017/ 0800751010
0 comments:
Post a Comment