Nafasi Ya Matangazo

March 28, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Luteni Mstaafu Chiku Gallawa kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshuhudia Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akiweka sahihi katika hati ya kiapo mara baada ya kuapa kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisaini hato ya kiapo cha Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
Rais  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi  Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe Samia suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim  na  Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016. Kulia ni mume wa mkuu huyo wa Mkoa Bw. Juma` Boma na kushoto ni bintiye.
***************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemwapisha Mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa, ambaye hakuapishwa pamoja na wakuu wa mikoa wenzake Machi 15, 2016.

Uapisho huo umefanyika leo tarehe 28 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Luteni Mstaafu Chiku Gallawa anakuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza kwa Mkoa mpya wa Songwe, ulioanzishwa kwa kuugawa mkoa wa Mbeya, Kusini mwa Tanzania.

Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amepokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Rais Magufuli amepokea taarifa hiyo yenye ripoti tano, ikiwa ni utaratibu wa kikatiba unaomtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kukabidhi kwa Rais taarifa ya ukaguzi kabla ya mwisho wa mwezi Machi.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Magufuli ataikabidhi mbele ya bunge katika siku saba za mwanzo za kikao kijacho cha Bunge kitakachofanyika Mjini Dodoma.


Rais Magufuli amempongeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali na timu yake kwa kuandaa taarifa hiyo, na ametoa wito kwa chombo hicho kuendelea kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi, huku akiahidi kuwa serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kazi zake.
Posted by MROKI On Monday, March 28, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo