Maofisa ya TBL Group na Syngeta Tanzania wakiwa katika
picha ya pamoja katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usalama kwa
wakulima iliyofanyika mwishoni mwa wiki, kutoka kushoto ni Boniface
Dickson (Afisa Mauzo wa Syngeta),Godwin Mollel (Mwenyekiti wa chama cha
wakulima wa Shahiri cha Fungamano),Benson Sangale (Afisa Kilimo wa TBL Group),
Francis Ndeithi (Afisa wa Syngeta),Mohamed Matingas na Paul Antapa wote wawili
maafisa kilimo wa TBL Group
******************
KATIKA utekelezaji zaidi wa kanuni za usalama kazini kampuni ya TBL
Group imetangaza kuwa itaanza kuwapatia wakulima wa zao la shahiri
wanaoshirikiana na kampuni hiyo mkoani Arusha na Kilimanjaro vifaa vya usalama ili kuwawezesha
kufanya kazi yao mashambani wakiwa katika hali ya usalama.
Akizungumza wakati
wa hafla ya kupokea vifaa vya usalama wa wakulima kutoka kampuni ya kuuza
madawa na pembejeo za
kilimo ya Syngenta
Tanzania ,Meneja Kilimo wa TBL Dk. Bennie Basson , alisema kuwa TBL Group siku zote imekuwa
kinara kwa kuzingatia usalama kazini kwa wafanyakazi wake na sasa kanuni hizo
pia itahakikisha zinatekeleza kwa wakulima inaoshirikiana nao sehemu mbalimbali
nchini. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
“Wakulima wengi
nchini siku hizi wanatumia madawa ya kuua wadudu wanaoharibu mazao na mbolea za kisasa mashambani na mara
nyingi wamekuwa
wakipata athari mbalimbali zinazotokana na kemikali zisizo rafiki kwa miili yao
hivyo ni muhimu kutumia vifaa vya kuwakinga wasipate madhara na kuwapatia elimu
juu ya matumizi sahihi ya madawa hayo,”alisema,Dk Basson.
Aliongeza kuwa zaidi ya wakulima 700,000 wanaotumia madawa ya kemikali
katika mikoa mbalimbali wako hatarini kupata madhara yatokanayo na madawa ya
kilimo yenye sumu kutokana na kutokuwa na vifaa vya kuwakinga na aliipongeza kampuni ya
Syngenta Tanzania kuanzisha utaratibu wa kutoa vifaa vya kinga kwa wakulima na
kuyataka makampuni mengine yanayouza madawa ya kilimo na pembejeo za kilimo
kuiga mfano huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Syngeta nchini, Samwel Muturi, alisema kampuni yake ikiwa inafanya kazi na wakulima
ambao ni wanunuzi wakuu wa bidhaa zake imeona kuna umuhimu wa kuwapatia pia
vifaa vya kuwakinga wawe salama na imeamua kuanza na wakulima wa zao la Shahiri
wanaoshirikiana na TBL Group mkoani Arusha na itaendeleza utaratibu huo sehemu
mbalimbali nchini.
Naye Mwenyekiti wa kikindi cha uzalishaji wa zao la Shahiri cha
Fungamano cha Arusha,Godwin Mollel akiongea kwa niaba ya wakulima wenzake alishukuru
kwa wakulima
kufikishiwa vifaa vya kinga ambavyo vitawawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi
wakati huohuo kutopata madhara ya kiafya.
“Tunatoa shukrani kwa kampuni ya TBL Group ambayo imekuwa mstari wa
mbele kusaidia wakulima wa Shahiri inaoshiikiana nao ,kwa kiasi kikubwa
wakulima wengi tumeweza kuwa na maisha bora kutokana na ushirikiano huu na tuna
imani ukiendelea tutazidi kuiga hatua za maendeleo na kuwa na maisha mazuri
zaidi,”alisema Mollel.
0 comments:
Post a Comment