Mwenyeki wa kamati John Nayopa
akimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo,Taarifa ya kamati
ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa
Nyamongo na Kampuni ya mgodi wa dhahabu ya Acacia North Mara,
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo,akionesha taarifa aliyokabidhiwa na Kamati hiyo ambapo
ameahidi kuisoma na kuitolea majibu yanayostahili ndani ya kipindi cha wiki
tatu tangu Machi 23,2016 alipokabidhiwa taarifa hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya
kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa
Nyamongo na Kampuni ya mgodi wa dhahabu ya Acacia North Mara, John Nayopa,
akisoma taarifa ya utekelezaji wa kamati hiyo mbele ya Waziri wa Nishati na
Madini( hayupo pichani)
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, akizungumza jambo mara baada ya kupokea Taarifa ya utekelezaji kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North Mara katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara na Mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa North Mara.
Meza kuu ikimsikiliza
Mwenyekiti wa Kamati( hayupo) akitoa taarifa ya utekelezaji ya Kamati ya
kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North
Mara katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara na Mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa
North Mara, kutoka kushoto waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter
Muhongo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga, Mbunge wa Tarime Vijijini
John Heche.
Sehemu ya wajumbe kutoka
Serikali za vijiji wakisikiliza taarifa ya kamati ya kushughulikia mgogoro kati ya
wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North Mara katika eneo la Nyamongo
Wilayani Tarime Mkoani Mara na Mgodi wa
dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa North Mara, kutoka Serikali ya kijiji.
Sehemu ya wajumbe kutoka Mgodi
wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa North Mara, wakisikiliza taarifa ya Kamati
ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa
North Mara katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara na Mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa
North Mara. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Sehemu ya ya wanakamati
wakisikiliza taarifa ya utekelezaji kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya
kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North
Mara katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara na Mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa
North Mara.
******************
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo amepokea ripoti maalumu ya kumaliza mgogoro wa wananchi
wa Nyamongo na mgodi wa wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia North Mara uliodumu kwa
miaka 6 sasa. Anaandika Zuwena Msuya-Wizara ya Nishati na Madini.
Akizungumza mjini Tarime Mkoani Mara baada ya kupokea ripoti hiyo Prof. Muhongo ameshauri wananchi wa Tarime kuwa watulivu wakati akiendelea kuisoma ripoti hiyo na kutolea majibu mambo yalioyo andikwa katika riporti hiyo.
Profesa Muhongo alisema anaimani mambo yote yalioandikwa katika ripoti hiyo ni mawazo ya wananchi waliohojiwa na atashangaa endapo kuna mtu atajitokeza kuikataa.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya
Tarime,Glorious Luoga alisema ripoti hiyo itatoa majibu stahiki kwa wanaohitaji
kulipwa na hata wasiostahili hivyo wananchi wakae tayari kupokea utekelezaji wa
ripoti baada ya kusoma na kupitishwa na Waziri.
Naye Mbunge wa Tarime vijijini John Heche
alisema kuwa anaimani na ripoti hiyo kuwa itatenda haki kwa wananchi wake wa
Nyamongo ili kutimiza ahadi ya Rais aliyoitoa wakati akiomba kura kuwa
hatamaliza kabisa tatizo la Nyamongo lililodumu kwa muda mrefu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhandisi John Nayopa alisema kamati hiyo imepokea malalamiko zaidi ya 4400 ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi,malalamiko ambayo yalilenga masuala ya fidia ya ardhi,athari za shughuli za mgodi hasa upande wa mazingira,uvamizi wa mgodi,sakata la tegesha na Askari kutuhumiwa na kunyanyasa na kutesa wananchi.
Kamati hiyo iliundwa na Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mwezi mmoja uliopita ina wajumbe
27,19 wataaalamu wa Serikali, na Wenyeviti wa vitongoji 80.
0 comments:
Post a Comment