Meneja wa Dawasco llala (katikati) Mhandisi Ramadhani Mtindasi pamoja na mjumbe wa mtaa wa Kota Bi. Habiba Hamisi akionyesha bomba la Maji ambalo linaleta Maji kutoka kwenye laini kuu lilo uunganishwa kiholela inayotoka kwenye Bomba kubwa kwenye eneo la Ilala Kota Mchikichini Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Dawasco Ilala Mhandisi Ramadhani Mtindasi akionyesha boza linalotumika kuhifadhi Maji yanayotoka kwenye bomba la Dawasco .
*************
SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Jijini Dar es Salaam
(Dawasco) limebaini wizi mkubwa wa Maji kwenye unaofanywa na wamiliki wa
magorofa kujiunganishia maji ya dawasco bila kufuata utaratibu.
Katikia operesheni ya kuwasaka wezi wa maji na waharibifu
wa miundombinu yake iliyofanyika juzi katika mtaa wa Ilala Kota karibu na
nyumba za Shirika la nyumba la taifa (NHC) jijini Dar es Salaam ilibaini kuwepo
kwa watu waliojiunganishia maji kinyume cha sheria.
Akizungumza kwenye tukio hilo Meneja wa Dawasco Ilala,
Ramadhani Mtindasi alieleza kuwa wanatekeleza agizo la Waziri wa Maji ambapo
amewaagiza Dawasco kufunya uchunguzi kwenye Majengo makubwa na viwanda jijini
ambayo wanadai wanatumia Maji ya visima na ndipo walipogundua jengo hilo la
ghorofa lenye nyumba ndogo (apartments) 8 likiwa na laini mbili moja ya Maji ya
kisima na nyingine ni ya Dawasco ambayo haikuwa na mita wala kusajiliwa na
Dawasco . SOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
“Tumeanza operesheni maalum ya kukagua majengo
yote makubwa jijini ambayo wanatumia huduma ya Maji ili kubaini kama ni ya
visima au ya Dawasco kama Waziri wa Maji alivyotuagiza na ndipo tulipogundua
jengo moja eneo la Ilala Kota likiwa na laini ya Maji ya Dawasco ila halina
mita wala hatujamsajili amejiunganishia kiholela,”alisema Mtindasi.
Hata hivyo mmiliki wa jingo hilo hakuwepo na
alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa yeye hutumia maji ya kisima lakini
Dawasco walimtaka kufika ofisini kwani alikuwa ana line mbili ya kisima na
bomba la dawasco.
Mjumbe wa Mtaa huo wa Ilala Kota, Habiba Hamisi ambaye
alikuwepo katika msako huo alisema kuwa Majengo mengi makubwa yamekuwa
yakijiunganishia huduma ya Maji kiholela na kudai kuwa ni ya kisima kumbe sio
hivyo kuwafanya wananchi wengine waotegemea huduma ya Maji ya Dawasco kukosa
kutokana na kuwa majengo hayo makubwa yana matumizi makubwa.
“Majengo mengi makubwa yana laini mbili ya Dawasco
na visima ila ukiwauliza wanasema wanatumia maji ya visima tu kumbe sio kweli
na matumizi yao kwenye majengo hayo ni makubwa hivyo wanasabisha wanaostahili huduma
hiyo kukosa maji hivyo Dawasco wawachukulie hatua kali za kisheria” alisema Hamisi.
Dawasco imewasihii wamiliki wote wa majengo
makubwa ambao wamejiunganishia huduma ya Maji Kiholela kujisalimisha mapema
kabla ya hatua kali za kisheria hazijachukuliwa juu yao endapo watakamatwa.
0 comments:
Post a Comment