Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier
Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika
Mashariki, Javier Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja
na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier
Rielo.
**********
Makamu wa Rais wa
Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo amemuhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi
wa bomba la kusafirisha Mafuta kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga hapa
Tanzania haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.
Bw. Javier Rielo
ametoa ahadi hiyo leo tarehe 14 Machi, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo
na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mradi huo
utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha
mafuta ghafi mapipa 200,000 kwa siku kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari
ya Tanga na utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za
moja kwa moja 20,000.
Katika Mazungumzo
hayo Bw. Javier amemueleza Rais Magufuli kuwa Kampuni yake inatarajia kutumia
dola za kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari zimeshaandaliwa.
Pamoja na
kuukaribisha uwekezaji huo mkubwa kwa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka
kampuni hiyo kuharakisha mchakato wa kuanza kwa mradi, na ameshauri muda wa
miaka mitatu uliopangwa kuukamilisha mradi huo upunguzwe, ili manufaa yake
yaanze kupatikana mapema.
Kwa upande wake
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, amesema Wizara yake ipo
tayari kuhakikisha mradi huo unafanikiwa, na itatoa ushirikiano wa kutosha
kuharakisha utekelezaji wake.
Prof. Muhongo
amebainisha kuwa licha ya kwamba hali ya kijiografia, hali ya hewa na bandari
ya Tanga vinatoa mazingira bora ya kufanikiwa kwa mradi huo, Tanzania pia
inatarajia kunufaika na bomba hilo, kwa kuwa kuna tafiti mbili za mafuta zinazoendelea
katika ziwa Tanganyika na ziwa Eyasi, ambazo zikikamilika kwa mafanikio
inatarajiwa bomba hilo litasaidia kusafirisha mafuta yake.
0 comments:
Post a Comment