Nafasi Ya Matangazo

March 14, 2016

Meneja wa Dawasco llala (katikati) Mhandisi Ramadhani Mtindasi pamoja na mjumbe wa mtaa wa Kota Bi. Habiba Hamisi akionyesha bomba la Maji ambalo linaleta Maji kutoka kwenye laini kuu lilo uunganishwa kiholela inayotoka kwenye Bomba kubwa kwenye eneo la Ilala Kota Mchikichini Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Dawasco Ilala Mhandisi Ramadhani Mtindasi  akionyesha boza linalotumika kuhifadhi Maji yanayotoka kwenye bomba la Dawasco .
*************
SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Jijini Dar es Salaam (Dawasco) limebaini wizi mkubwa wa Maji kwenye unaofanywa na wamiliki wa magorofa kujiunganishia maji ya dawasco bila kufuata utaratibu.

Katikia operesheni ya kuwasaka wezi wa maji na waharibifu wa miundombinu yake iliyofanyika juzi katika mtaa wa Ilala Kota karibu na nyumba za Shirika la nyumba la taifa (NHC) jijini Dar es Salaam ilibaini kuwepo kwa watu waliojiunganishia maji kinyume cha sheria.

Akizungumza kwenye tukio hilo Meneja wa Dawasco Ilala, Ramadhani Mtindasi alieleza kuwa wanatekeleza agizo la Waziri wa Maji ambapo amewaagiza Dawasco kufunya uchunguzi kwenye Majengo makubwa na viwanda jijini ambayo wanadai wanatumia Maji ya visima na ndipo walipogundua jengo hilo la ghorofa lenye nyumba ndogo (apartments) 8 likiwa na laini mbili moja ya Maji ya kisima na nyingine ni ya Dawasco ambayo haikuwa na mita wala kusajiliwa na Dawasco . SOMA ZAIDI BOFYA HAPA.

 “Tumeanza operesheni maalum ya kukagua majengo yote makubwa jijini ambayo wanatumia huduma ya Maji ili kubaini kama ni ya visima au ya Dawasco kama Waziri wa Maji alivyotuagiza na ndipo tulipogundua jengo moja eneo la Ilala Kota likiwa na laini ya Maji ya Dawasco ila halina mita wala hatujamsajili amejiunganishia kiholela,”alisema Mtindasi.

Hata hivyo mmiliki wa jingo hilo hakuwepo na alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa yeye hutumia maji ya kisima lakini Dawasco walimtaka kufika ofisini kwani alikuwa ana line mbili ya kisima na bomba la dawasco.

Mjumbe wa Mtaa huo wa Ilala Kota, Habiba Hamisi ambaye alikuwepo katika msako huo alisema kuwa Majengo mengi makubwa yamekuwa yakijiunganishia huduma ya Maji kiholela na kudai kuwa ni ya kisima kumbe sio hivyo kuwafanya wananchi wengine waotegemea huduma ya Maji ya Dawasco kukosa kutokana na kuwa majengo hayo makubwa yana matumizi makubwa.

“Majengo mengi makubwa yana laini mbili ya Dawasco na visima ila ukiwauliza wanasema wanatumia maji ya visima tu kumbe sio kweli na matumizi yao kwenye majengo hayo ni makubwa hivyo wanasabisha wanaostahili huduma hiyo kukosa maji hivyo Dawasco wawachukulie hatua kali za kisheria” alisema Hamisi.


Dawasco imewasihii wamiliki wote wa majengo makubwa ambao wamejiunganishia huduma ya Maji Kiholela kujisalimisha mapema kabla ya hatua kali za kisheria hazijachukuliwa juu yao endapo watakamatwa. 
Posted by MROKI On Monday, March 14, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo