Bomba la Maji lilounganishiwa kiholela ambalo halina mita linalopeleka huduma ya Maji kwenye jengo kubwa la ghorofa ambalo linamilikiwa na Chuo cha Biashara (CBE) eneo la Oysterbay mtaa wa Msasani Rd Jijini Dar es Salaam.
Maofisa wa Dawasco Kinondoni waking’oa laini ya Bomba la Maji lilounganishiwa kiholela lisilo na Mita kwenye jengo kubwa la ghorofa linalomilikiwa na Chuo cha Biashara (CBE) eneo la Oysterbay mtaa wa Msasani Rd Jijini Dar es Salaam.
****************
Shirika la maji safi na maji taka Dar es Salaam
(Dawasco) limeendeledea na msako wake wa kubaini wezi wa maji na waharibifu wa
miundombinu yake jijini Dar es Salaam na safari hii limeingia Oysterbay
Wilayani Kinondoni na kubaini wizi wa maji kwenye majengo makubwa.
Katika msako uliofanyika Oysterbay Mtaa wa
Msasani, jijini Dar es salaam na kuongozwa na Meneja wa Dawasco Kinondoni, Judith
Singinika walibaini kuwepo kwa wizi wa maji katika jingo la ghorofa mali ya
Chuo cha Biashara (CBE) katika jingo lake lenye makazi 25.
Singinika alisema kuwa operesheni hiyo maalum
inayoendelea ni utekelezaji wa agizo la waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson
Lwenge la kuwataka Dawasco kukagua majengo yote makubwa na viwanda juu ya
matumizi yao ya maji.
“Tunaendelea na utekelezaji wa agizo la Waziri
la kukagua majengo yote makubwa pamoja
na viwanda Jijini Dar es Salaam ilikubaini vyanzo vyake vya Maji ,ndipo tulipobaini wizi mkubwa wa maji
mtaa wa Msasani Road kwenye jengo hilo la ghorofa lenye nyumba ndogo(apartments)
25 linalomilikiwa na CBE ambapo
kulikutwa na laini mbili zinazoleta Maji
na laini moja ikiwa haina mita na ndiyo ilikuwa inafanyiwa atumizi makubwa,”alisema
Singinika.
Singinika alisema wamechukua hatua za kisheria kwa
kukitoza chuo hicho faini ya Shilingi milioni 100 ambapo inatakiwakulipwa ndani
ya miezi 24 hivyo kila mwezi wanatakiwa kulipa kiasi kisichopungua shilingi
milioni 4,160,000.
Dawasco inaendelea kuwasihi wamiliki wote wa
Majengo makubwa ya ghorofa pamoja na viwanda waliojiunganishia huduma ya Maji
kiholela kijisalimisha kwani operesheni hiyo ni endelevu na hatu kali za
kisheria zitachukuliwa kwa yoyote atakaye kamatwa.
0 comments:
Post a Comment