Nafasi Ya Matangazo

March 09, 2016

Kiungo  Haruma Moshi  Boban atalazimika kusubiri mpaka Marchi 14 kuingia tena kwenye kikosi cha City kufuatia kusumbuliwa na maralia jambo linalomfanya kuukosa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Stand United ya Shainyanga  uliopangwa  kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Sokoine  jijini hapa.

Muda mfupi uliopita  mkuu wa kitengo cha  utabibu kwenye kikosi cha City, Dr Joshua Kaseko ameifahamisha  mbeyacityfc.com kuwa mara baada ya kikosi kizima kurejea Mbeya kutoka jijini Dar kwenye mchezo wa ligi  dhidi ya Simba, alipata taaraifa ya kutokuwa katika hali nzuri kwa kiungo huyo na baada ya kumfanyia vipimo  aligundua  kuwa Boban ana  Maralia.

“Ni wazi hatakuwa sehemua ya mchezo kesho,ana Maralia tumeshamtaarifu mwalimu juu ya hili na tayari ameanza kufanya  mazoezi maalumu na yule atakayechukua nafasi yake, imani yangu kubwa kuwa atakuwa sehemu ya kikosi march 14 wakati tutakapokuwa tunacheza na Africans Sports jijini Tanga alisema.

Katika hatua nyingine  Dr Kaseko alidokeza  kuwa kiuongo mwingine wa kati, Kenny Ally Mwambungu ataukosa mchezo wa kesho kupisha kadi tatu za jano alizopata mfululizo kwenye michezo mitatu ya City iliyopita, na kukumbumbusha pia kuwa  mlinzi Deo Julius bado atakuwa nje ya kikosi akiendelea kuuguza majeraha ya goti.

“Kwenye mchezo wa kwesho pia tutawakosa Kenny Ally (pichani juu) na Deo Julius kutokana na sababu kadha wa kadha, Kenny amepata kadi tatu za njano mfululizo kwenye michezo yetu mitatu iliyopita na Deo bado hajapona majeraha ya goti hivyo nao hawatakuwa sehemu ya mchezo hapo kesho”alimaliza

City inakutana na Stand United hapo kesho kwenye uwanja wa Sokoine huu ukiwa ni mchezo wa nne kwa timu hizi huku rekodi ikionyesha timu hiyo ya Shinyanga kushinda mara mbili na City ikiwa imeshinda mara moja, hivyo mchezo wa  kesho unatarajiwa kuwa  na ushindani wa hali ya juu.


Aliyekuwa mshambuliaji wa City, Paul Nonga (sasa yupo Yanga) akishangilia mara baada ya kuifungia timu yake bao la pili kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Stand United msimu uliopita mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
Posted by MROKI On Wednesday, March 09, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo