Ukifika mkoani Mbeya eneo la Iyunga kilipo kiwanda cha kutengeneza bia
cha TBL na kufanikiwa kuingia kiwandani hapo utajisikia uko eneo tofauti
kutokana na mandhari utakayokutana nayo kuanzia majengo ya kiwanda ,mwonekano wa
wafanyakazi ambao wengi wao ni vijana, mazingira ya ndani ya kiwanda na
yaliyokizunguka bila kusahau mitambo ya kisasa ya uzalishaji iliyopo kiwandani hapo.
Kiwanda cha TBL tawi la Mbeya kilichopo chini ya kampuni ya TBL Group ni miongoni mwa viwanda bora vya
kutengeneza bia barani Afrika kinachoongozwa na msomi wa kitanzania mwenye fani
ya Uhandisi katika fani ya umeme wa Viwandani Mhandisi Waziri Jemedari.
Katika mahojiano yaliyofanyika hivi karibuni Mhandisi Jemedari ameeleza
kuwa anaipenda kazi yake na anajisikia furaha kuongoza kiwanda kikubwa cha TBL
Mbeya ambacho ni
miongoni mwa viwanda bora vya kutengeneza bia katika bara la Afrika kikiwa
kimeajiri hazina ya vijana wasomi wa kitanzania ambao wanamudu vizuri kazi zao.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Aliongeza kusema kuwa Kutokana na historia hii ya ubora barani Afrika,
kiwanda kimekuwa kikiendelea kufanya vizuri na kinavutia wageni kutoka sehemu mbalimbali ambao wamekuwa
wakikitembelea mara kwa mara kwa
ajili ya kujionea mafanikio na kujifunza.
Siri ya kiwanda hiki kuwa kiwanda bora alisema kuwa kilipoanzishwa kilifungwa vifaa na
mitambo ya kisasa ya uzalishaji vilevile kilianza kutumia kanuni bora za
uendeshaji viwanda kwa njia ya kisasa za kampuni ya SABMiller ambayo ndiyo
inamiliki kampuni mama ya TBL Group.
Alisema kanuni hizi zinazojulikana kitaalamu kama The Manufacturing Way zinaelekeza mfumo wa uzalishaji bora wenye
viwango na wenye kuleta tija,na kugusa maeneo yote ya uendeshaji viwanda kwa ufanisi wenye kuleta matokeo bora
na zikifuatwa na kutekelezwa ipasavyo lazima matokeo yake yawe mazuri na
mafanikio yapatikane.
“TBL Group hivi
sasa inatumia kanuni hizi katika viwanda vyake vyote na matokeo yake
yanaonekana kuanzia kwenye uchangiaji wa pato la taifa kupitia kodi,kuwa
mwajiri bora,kusaidia masuala mbalimbali ya kijamii,kuwezesha wakulima
wanaouzia kampuni malighafi za kutengenezea vinywaji,kuzingatia kanuni za
usalama kazini,kupunguza tatizo la ajira nchini na mengineyo mengi”.Alisema.
Pia alisema mfumo huu unaenda sambamba na kampuni kuajiri vijana wa
kitanzania ambao wanapatiwa fursa ya kuonyesha vipaji vyao na wanaendelezwa kwa
kupatiwa mafunzo mbalimbali ambapo wanafanya kazi kwa ufanisi na kuleta matokea
mazuri “TBL Group ni tanuru la kuendeleza vipaji na ina mfumo wa kuajiri wafanyakazi waliobobea kwenye
fani mbalimbali ambao wanaendana na viwango vya kampuni na mchango wao na
ufanisi wao katika kazi kuongeza mafanikio.
Kuhusiana na historia yake Jemedari anasema kuwa ni Mzaliwa wa mkoani Mara ambaye alipata elimu ya msingi na sekondari na baadaye
kujiunga na.Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisomea shahada ya kwanza ya
Uhandisi wa umeme.
Mbali na shahada ya Uhandisi akiwa mwajiriwa wa TBL amehudhuria kozi
mbalimbali nje ya nchi ambazo zimezidi kumpatia maarifa katika fani yake na
kumfanya awe miongoni mwa wahandisi nguli wanaoaminika nchini katika fani ya
umeme wa viwanda hususani vinavyozalisha vinywaji.
Baadhi ya kozi ambazo zimemnoa zaidi kitaalamu alisema kuwa alizipata
katika nchi za Afrika
ya Kusini na nchini
Ujerumani bila kusahau mafunzo ya ndani anayoendelea kuyapata kiwandani hapo
kwa sasa
Kuhusiana na historia yake ya kazi anasema kuwa alijiunga na TBL
mwaka mwaka 1999 kama
mhandisi wa umeme na baada
ya kutumikia kiwanda hicho kwa kipindi kirefu akiwa ameshikilia nafasi
mbalimbali za uongozi kwenye idara yake. Alijiunga na kampuni ya Coca Cola
Kwanza kwa ajili ya kupata ujuzi zaidi ambako alifanya kazi kazi kwa muda mfupi
na kurejea tena TBL ambako anaendelea kufanya kazi hadi leo akiwa Meneja wa
Kiwanda.
Mafanikio aliyoyapata akiwa mfanyakazi wa TBL amesema kuwa ni mengi
ikiwemo kuhudumia familia yake vizuri pia amejifunza mambo mengi yanayomsaidia
kuendesha maisha na yatakayomsaidia kimaisha hata baada ya kustaafu kazi.
Kuhusu changamoto anazokabiliana nazo katika kazi yake alisema ni za
kawaida na anaamini kuwa hakuna kazi isiyokuwa na changamoto kinachotakiwa na
kuangalia namna ya kukabiliana nazo.
Mbali na kazi yake ya utawala na uhandisi umeme baada ya saa za kazi
anapendelea kusoma vitabu mbalimbali ikiwemo kujishughulisha na ufugaji
“Napenda sana shughuli za ufugaji na mara nitakapostaafu kazi nitakuwa mfugaji vilevile
kujishughulisha na utoaji wa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na fani yangu ya
umeme.
Jemedari anatoa wito kwa vijana wa kitanzania kutokimbia masomo ya
hesabu na sayansi wanapokuwa mashuleni bali wajitahidi kukomaa nayo kwa
kuwa katika dunia hii
ya sayansi na teknolojia bila wataalamu wa kutosha katika nyanja mbalimbali
itakuwa vigumu kwa taifa kupiga hatua ya maendeleo na pindi watakapoajiriwa au
kujiajiri wafanye kazi kwa bidii.
The Engineer...
ReplyDelete