WADAU mbalimbali,Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wanatarajia kukutana kwenye Mkutano Mkuu wa 25 wa mwaka wa mfuko huo kwaajili ya kujadili mambo mbalimbali yakiwemo ya uendelezaji wa sekta ya uhifadhi ya jamii.
Akizungumza na mtandao huu,jijini Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa taarifa hiyo, Meneja Uhusiano PPF, Lulu Mengele alisema kuwa mkutano huo utafanyika Februari 11 na 12 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini hapa,huku ukihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema pamoja na kujadili uendelezaji huo pia watajadili mafanikio ya mfuko huo kwa mwaka mzima na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko, huku Kaulimbiu ya mkutano huo ikiwa ni 'Uendelezaji wa Sekta ya Hifadhi Jamii na Umuhimu wa kuzingatia Mabadiliko'.
"Mkutano huo utafanyika na wadau mbalimbali wakiwemo Wenyeviti na wajumbe wa bodi, maofisa watendaji wakuu, wakurugenzi, wakuu wa vitengo, vyama vya waajiri, ambapo baadhi ya Wanachama watapata fursa ya kutoa ushuhuda kuhusu huduma za mfuko wa PPF" alisema Lulu
Wakati huohuo, Mengele alizungumzia mfumo maalumu wa Wote Scheme ambao unazihusisha sekta zisiyo rasmi na ule mfumo wa ziada uliopo kwenye sekta iliyo rasmi.
Alifafanua lengo kuu la mfumo huo kuwa ni kukidhi mahitaji na kutambua mchango na ushiriki wa sekta isiyo rasmi kwenye uchumi na pia kutoa fursa mbalimbali kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta rasmi ili kuwawezesha kunufaika na mfumo huo kwa ajili ya kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Kuhusu nani anastahili kujiunga , Mengele alisema kila mtu au kikundi chenye kipato na chenye mlengo wa kiuchumi kilichopo kwenye sekta isiyo rasmi kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, mama lishe, waendesha bodaboda, wajasiriamali, wadogo, wasanii, wanamichezo wachimbaji madini wadogo.
Ambapo alisema kuwa jinsi ya kuchangia kiwango cha chini kwa mwezi ni sh.20,000 ambacho kinaweza kulipwa aidha moja kwa moja kwenye akaunti ya Mfuko wa Pensheni wa PPF au kwa njia ya M-Pesa, Airtel money na Tigo pesa.
0 comments:
Post a Comment