Hivi karibuni Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Bi. Doris Mollel alitembelea ofisi za mchora vibonzo
nchini Nathan Mpangala na kufanya nae mazungumzo kuhusu namna vibonzo
vinavyoweza kutumika kuelimisha umma kuhusu watoto wanaozaliwa kabla ya wakati
maarufu kwa jina la Njiti.
Bi. Doris alisema baadhi ya sababu
zinazosababisha watoto njiti ni pamoja na pombe, dawa za kulevya, upungufu
wa damu mwilini, uzito mkubwa kwa mama mjamzito, uvutaji
sigara/bangi, magonjwa ya kisukari, presha, maambukizi, kifafa cha uzazi, matatizo kwenye cervix
inashindwa kujifunga na kujikaza kubeba mtoto, kondo (placenta) inapokuwa na
tatizo, kushika mimba haraka baada ya kujifungua mtoto mwingine, mimba ya
mapacha, chupa kupasuka kabla ya wakati, msongo wa mawazo, kazi ngumu, vipigo,
mimba za utotoni, mimba za uzeeni, kutopata vipimo sahihi na kwa wakati,
kutotumia vitamins/foilic acid, lishe nk.
0 comments:
Post a Comment