SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam
(DAWASCO), imerejesha huduma ya
upatikanaji wa Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini jijini Dar es salaam, pamoja na maeneo ya mji
wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 36
kuanzia siku ya Alhamisi 18/02/2016.
Akizungumzia kurejea kwa huduma hiyo, Meneja
uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amesema kuwa huduma ya Maji katika
jiji la Dar es salaam na miji ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa sasa yameanza kwenda
kwa wananchi, na maeneo mengi ya jiji ambayo yalikosa huduma ya Maji kutokana
na uzimwaji wa mtambo wa Ruvu chini.
“Napenda kuwaambia wateja wetu kuwa huduma ya Maji
kwa sasa imerejea kwenye maeneo mengi ya jiji baada ya matengenezo kukamilika na
mtambo kuwashwa siku ya Jumapili saa 9:30 alasiri” alisema Bi. Lyaro
Alibainisha kuwa Kuna maeneo mengine yatachelewa
kupata Maji kwani mara nyingi kwa kitaalamu huwa mtambo ukizimwa kwa zaidiya
saa 24 ndani ya mabomba ya kupitisha Maji hujaa hewa hivyo baadhi ya maeneo
kazi ya utoaji hewa kwenye mabomba unaendelea, hivyo tuwahakikishie wananchi
kuwa huduma imerejea na wataipata ndani ya muda tuliotarajia.
Awali, mtambo wa Ruvu Chini ulizimwa ili kuwaruhusu
wakandarasi kutoka kampuni ya sino Hydro na mafundi kutoka DAWASCO kukarabati
bomba la Maji lenye inchi 54 linalosafirisha Maji kutoka Bagamoyo mpaka matenki
ya Chuo kikuu cha ardhi, Bomba lililokuwa likivuja maeneo ya Makongo Jeshini,
na kusababisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kukosa huduma ya Maji,
Mji wa Bagamoyo vijiji vya Zinga, Kerege na Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta,
Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe.
Maeneo mengine ni pamoja na Maeneo ya Mlalakuwa,
Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni,
Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City centre, Ilala,, Ubungo Maziwa,
Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Muhimbili, Buguruni, Chang’ombe na Keko.
0 comments:
Post a Comment