Msajili wa Hazina, Lawrence
Mafuru (katikati), akikata tepe kikiwa ni ishara ya uzinduzi wa huduma za
kifedha kwenye tawi la Benki ya Posta Babati mkoani Manyara leo Februari 9,
2016. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, na kushoto
ni Menyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi YA tpb, Profesa Lettice Rutashobya.
Msajili wa hazina, Lawrence
Mafuru (wapili kushoto), akimpa zawadi mmoja wa wateja wa Benki ya Posta tawi
la Babati, Theofil Muhale Tsaghayo baada ya kufungua rasmi huduma za kibenki
katika tawi la Babati, mkoaniManyara Februari 9, 2016. kushoto ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Benki hiyo Prof. Lettice Rutashobya.
***************
Na Mwandishi wa K-VIS MEDIA,
Babati
Benki ya Posta Tanzania (TPB)
imezindua huduma za Kibenki kwa kufungua tawi lake jipya kwenye mji wa Babati
mkoani Manyara. Akizungumza kwenye uzinduzi huo Februari 9, 2016, Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa TPB, Lettice Rutashobya alisema tawi lililokuwepo hapo
awali halikuweza kutosheleza mahitaji ya wakazi wa Mji wa Babati na vitongoji
vyake kutokana na udogo wake.
‘’Tawi hili limefunguliwa ili
kutimiza dhamira ya Benki yetu ya kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na
wateja wake, na sasa Tawi hili litatoa huduma bora na za kisasa ikiwemo ile ya
ATM kwa wafanyabiashara, wafanyakazi na wananchi kwa ujumla katika wilaya hii
ya Babati”, aliwahakikishia Profesa Rutashobya.
Profesa Rutashobya
aliwashukuru wateja wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake kwa kutumia
huduma wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake kwa kutumia huduma za
Benki hiyo kwa wingi, na kulifanya tawi hilo kuwa ni mojawapo ya matawi
yanayofanya vizuri kifaida.
Naye Msajili wa Hazina,
Lawrence N. Mafuru, ambaye ndiye aliyezindua huduma za kibenki za tawi hilo,
aliipongeza Benki ya Posta kwa kuleta maendeleo ya kuninua maisha ya Mtanzania
ya hali ya chini kwa kuongeza huduma za kibenki karibu na jamii hiyo, na kwa
kubuni huduma mbalimbali hususan za mikopo, zenye lengo la kumuinua kimapata
mwananchi wa chini.
Msajili huyo wa Hazina,
alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wakazi wa Babati kuchangamkia fursa
zinazotolewa na Benki ya Posta, kwa kufungua akaunti na kwenda kuomba mikopo
ambayo oinatolewa kwa riba nafuu na benki hiyo.
Kwa upande wake, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi amesema uamuzi wa kujenga
tawi hilo ambalo linatoa huduma zote zinapatikana kwenye matawi mengine ya
Benki ya Posta Tanzania nchi nzima.
“Azma ya Benki ya Posta, ni
kuwafikia na kutoa huduma za kibenki kwa wananchi wote (financial Inclusion),
alisema Moshingi.
0 comments:
Post a Comment