Wananchi wa Mkoa wa Geita wameaswa kufuata kanuni za usafi wa mazingira ili kudhibiti maumbukizi ya ugonjwa wa kipindupindu,Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea kambi ya kipindupindu iliyopo kwenye kituo cha afya cha Nyankumbu,mkoani hapa
Waziri Ummy akivaa vifaa maalum vya kujikinga na kipindupindu kabla ya kuingia kwenye kambi hiyo,kulia ni Mganga mfawidhi wa Kituo hicho Josephat Msafiri.(Picha Zote na Catherine Sungura WAMJW-GEITA)
Waziri Ummy akivua vifaa hivyo mara baada ya kutoka kuwasalimia wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi hiyo,wagonjwa waliopo hadi leo mchana ni wagonjwa wanneoWaziri huyo akiongea na mmoja wa wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi hiyo
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasalimia wagonjwa wa kipindupindu(hawapo pichani)kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt.Joseph Kisala
Baadhi ya wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi ya kituo cha afya cha Nyankumbu
0 comments:
Post a Comment