Nafasi Ya Matangazo

January 04, 2016

Wataalum kutoka Wizara ya Nishati  na Madini , Wizara ya kilimo ,uvuvi na mifugo, Wizara ya maji na umwagiliaji pamoja na watalaam kutoka bonde la mto Rufiji wakipita eneo ambalo kumejengwa tuta ili kuzua njia ya asili ya moja ya mito inayomwaga maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji kwa nia ya kupisha ujenzi wa mfereji wa maji yatakayotumika katika kilimo cha umwagiliaji, jambo ambalo  limedaiwa kuwa huathiri mazingira na utiririshaji wa maji katika mabwawa.
Cable wire za Umeme zikipitishwa katika moja ya njia zililizopo chini ya  mwamba wa mlima (tannel) ambapo ndipo zilizopo mashine za kuzalisha umeme wa maji na shughuli zote za uzalishaji.
Mashine  za kuzalisha umeme wa maji katika vituo vya Kihansi, kidato na Mtera  vinanyonekana ambapo shughuli zote za uzalisha wa umeme wa maji na mashine hizo ziko chini ya mwamba wa mlima uliotombelea .
Sehemu iliyochepushwa maji kitaalamu kutoka katika moja ya mito inayomwaga maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ili maji hayo  yatumike kwa kilimo cha umwagiliaji.
Tuta lilijengwa katika njia asili ya mto ili kupisha ujenzi wa mfereji wa maji yatakayotumika katika kilimo cha umwagiliaji, jambo ambalo  limedaiwa kuwa huathiri mazingira na utiririshaji wa maji katika mabwawa.
Posted by MROKI On Monday, January 04, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo