Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa George B. Simbachawene (Mb)
TAARIFA
KWA UMMA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa George B. Simbachawene
(Mb) amewasimamisha kazi Wakurugenzi Watendaji wa Manispaa za Kigoma, Mkoa wa
Kigoma na Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kuridhia na
kutekeleza maamuzi ambayo yamesababishia Serikali hasara na upotevu wa fedha.
Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kigoma Mhandisi Boniface Nyambele
anakabiliwa na tuhuma ya uuzaji wa nyumba za Halmashauri bila kufuata Sheria,
Kanuni na Taratibu zilizopo na bila kibali cha Waziri Mwenye Dhamana kama
Sheria inavyo elekeza.
Mkurugenzi wa Manispaa ya
Mpanda Ndugu Suleiman Lukanga ana
kabiliwa na tuhuma za Ununuzi hewa wa gari la kusomba taka kwa kiasi cha
shilingi milioni tisini na mbili na laki saba na elfu hamsini (92,750,000/=) na ubadhirifu wa fedha
za ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kakese kiasi cha shilingi milioni mia
mbili, tisini na nne (294,000,000/=).
Aidha, Mheshimiwa Waziri
wa Nchi ameagiza nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ikaimiwe na Mhandisi Sultan Imari Ndilowa ambaye ni
Mkuu wa Idara ya Maji, Manispaa ya Kigoma, nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya
Mpanda ikaimiwe na Ndugu Lauteri John Kanoni
ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Mheshimiwa Waziri wa Nchi,
amewataka Wakurugenzi Watendaji wa
Mamlaka za Serikali za Mitaa kote Nchini kuwa makini katika kutekeleza majukumu
yao wafuate Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.
Serikali haitasita kuchukua hatua za
kinidhamu kwa watumishi wote ambao watakiuka matakwa ya Sheria, Kanuni na
Taratibu na kutoweka mbele maslahi ya Umma.
Imetolewa
na:
Kitengo
Cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi
ya Rais – TAMISEMI.
Tarehe
18 Januari, 2016
0 comments:
Post a Comment