Balozi
wa Japan nchini, Masaharu Yoshida akisoma hotuba wakati wa halfa ya
kusaini mikataba ya msaada kutoka kwa serikali ya Japan, halfa
iliyofanyika kwa balozi jijini Dar es Salaam.
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Serikali
ya Japan kupitia mfuko wake wa misaada wa Grant Assistance for
Grassroots Human Security Projects (GGHSP) imesaini mkataba wenye
thamani ya Dola 204,300 sawa na Milioni 430 za Kitanzania kwa ajili ya
kusaidia miradi mitatu ya kijamii.
Akisoma hotuba katika halfa ya
kusaini mikataba hiyo ambapo Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Mhe.
Edward Lowassa alikuwa mgeni rasmi, balozi wa Japan nchini, Masaharu
Yoshida alisema serikali ya Japan imetoa msaada huo kwa kutambua
changamoto zilizopo katika sehemu ambazo wanatoa msaada huo na
wanataraji utaleta mabadiliko.
Balozi
wa Japan nchini, Masaharu Yoshida akikabidhiana mkataba na Mkurugenzi
wa Manispaa ya Morogoro, Theresia Mahongo baada ya kusaini mkataba huo
wenye thamani ya Dola 86,182 sawa na Milioni 180 za Kitanzania kwa ajili
ya ujenzi katika Shule ya Kingolwira.
Alisema licha ya miradi
ambayo serikali yake ya Japan imeweka saini kusaidia shughuli mbalimbali
za maendeleo, serikali ya nchi hiyo itaendelea kutoa misaada kwa
Tanzania kupitia mfuko huo ili kuzidi kupatikana kwa huduma bora kwa
watanzania.
“Ninayo furaha kusaini mikataba mipya mitatu ya
misaada kutoka serikali ya Japan kupitia mfuko wa Grant Assistance for
Grossroots Human Security Projects (GGHSP).
“Serikali ya Japan
itaendelea kutoa misaada katika kusaidia upatikanaji wa huduma za msingi
kwa Tanzania kupitia mfuko wa misaada na nimatumaini yangu sherehe ya
leo itazidi kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Japan,”
alisema Yoshida.
Balozi
wa Japan, Masaharu Yoshida na Askofu Solomon Massangwa kutoka Arusha
Lutheran Medical Centre wakikabidhiana mikataba baada ya kusaini mkataba
wa msaada kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Lutheran Arusha. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Aidha
Yoshida aliitaja miradi hiyo kuwa ni upanuzi wa Shule ya Msingi ya
Kingolwira ambayo mradi utasaidia ujenzi wa madarasa matatu , ofisi ya
mwalimu mkuu na jengo la choo ambapo mradi huo utagharimu Dola za
Kimarekani 86,182 sawa na Milioni 180 za Kitanzania.
Mradi wa pili ni ujenzi wa uzio katika
Shule ya Msingi Muyuni iliyopo Mkoa wa Kusini Unguja ambapo mradi
uagharimu Dola za Kimarekani 29,799 sawa na Milioni 62 za Kitanzania na
mradi wa tatu kuwa ni ununuzi wa vifaa katika hospitali ya Arusha
Lutheran Medical Centre wenye thamani ya Dola za Kimarekani 88,319 sawa
na pesa ya Kitanzania Milioni 185.
Akizungumza na Mo Dewji Blog
baada ya kusaini mikataba hiyo, mwakilishi wa Arusha Lutheran Medical
Centre, Askofu Solomon Massangwa alisema msaada ambao umetolewa na
serikali ya Japan utatumika kununua vifaa vya chumba cha wagonjwa
mahututi (ICU).
Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida akisaini mkataba pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa TCRA, Dkt. Ally Simba ambaye alimwakilisha mwalimu mkuu wa
Shule ya Muyuni katika halfa ya kusaini mkataba wenye thamani ya Dola
29,799 sawa na Milioni 62 za Kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa uzio
katika Shule ya Muyuni iliyopo mkoa wa Kusini Unguja.
Alisema
kwa mwaka 2014 kituo hiyo ilikuwa ikipokea hadi wagonjwa 9000 wa nje na
imekuwa ikipokea hadi wagonjwa kutoka nje za nje kama Kenya na hivyo
ununuzi wa vifaa hivyo vitasaidia kuwahudumia wagonjwa wanaofika katika
kituo hicho cha afya wakiwa mahututi.
“Wametupatia msaada wa wa
vifaa vya kwenye vyumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na tunawashukuru
sana kwa msaada huo na tunaamini utasaidia kuokoa maisha ya wananchi
wengi wanaofika kituoni kwetu kupata matibabu,” alisema Askofu
Massangwa.
Balozi
wa Japan, Masaharu Yoshida akiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi
katika halfa hiyo, Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Edward Lowassa wakati
kusaini mikataba ya miradi mitatu yenye thamani ya Dola 204,300 sawa
Milioni 430 ya Kitanzania kwa ajili kusaidia Shule ya Kingolwira, Shule
ya Muyuni na Kituo cha Afya cha Lutheran kilichopo Arusha.
Nae
mwakilishi wa Shule ya Kingolwira, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro,
Theresia Mahongo alisema msaada huo watatumia kama jinsi umevyokusudiwa
kwa kujenga majengo mapya lakini pia kutengeneza madawati ili kupunguza
tatizo hilo shuleni hapo na kuwataka wadau wa elimu mkoani Morogoro
kujitoa kusaidia sekta ya elimu mkoani humo.
Nae Mwalimu Mkuu wa
Shule ya Mbuyuni, Saleh Hamad alisema msaada huo umewafikia kwa muda
muafaka kipindi ambacho wamekuwa na mahitaji makubwa ya ujenzi wa uzio
katika shule hiyo kutokana na mazingira yaliyopo shuleni hapo na hivyo
kuishukuru serikali ya Japan kwa msaada imeowapatia na kuahidi kuitumia
kama walivyokusudia kutumika.
0 comments:
Post a Comment