MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege nchini
(TAA), Suleiman Suleiman amefariki dunia akiwa katika mazoezi ya
kuogelea katika Bahari ya Hindi, eneo la Kigamboni jijini Dar es
Salaam.
Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa
TAA, Ramadhan Maleta, alisema Mhandisi Suleiman alifikwa na mauti leo
asubuhi kwa kukosa nguvu wakati akiwa anaogelea .
Maleta, amesema ni kawaida ya Suleiman kufanya mazoezi
ya mwili kila siku kabla ya kwenda kazini na miongoni mwa mazoezi hayo ni kuogelea
ambapo leo kati ya saa 12:00 na saa 1:00 asubuhi ,akiwa anaogelea, mmoja wa
aliokuwa ameongozana nao, alibaini kuwa amekosa nguvu akiwa majini.
Baada ya kuomba msaada wa kumtoa majini na kumpa huduma ya
kwanza walimkimbiza Hospitali ya Aghakan kwa ajili ya matibabu lakini kabla ya
kufika walibaini amesha poteza maisha.
Mwili wa Marehemu Suleiman ambaye aliwahi pia kuwa Katibu wa
Klabu ya Simba ulitaraji kuzikwa leo jioni katika Makaburi ya Kisutu Dar es
Salaam.
Wakatihuohuo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa klabu ya Simba SC, kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo miaka ya 1998-2000 Seleman Said ‘Yeltisn’ kilichotokea leo jijini Dar es salaam.
Katika salamu hizo TFF imesikitishwa na kifo cha kiongozi huyo, ambaye alingoza klabu ya Simba SC na kupelekea kupewa jina la utani la ‘Yelstin” kutokana na ufanisi wake katika kazi na misimamo akifananishwa na aliyekua Rais wa kwanza Urusi wakati huo Boris Yeltsin.
TFF kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini inawapa pole familia ya Seleman Said ‘Yelstin’ ndugu jamaa, marafiki, uongozi na wanachama wa klabu ya Simba kufuatia kifo hicho, na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo.
Mazishi ya marehemu Selaman Said ‘Yelstin’ yanafanyika leo saa 10 kamili jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Marehemu Suleiman ameacha mke na
watoto watatu.
MUNGU
AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN
0 comments:
Post a Comment