Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wanne kutoka kushoto),
akimkabidhi kijana Diana Mosha, msaada wa vifaa mbali mbali vya
kutengenezea keki kupitia mpango wa Airtel ‘FURSA Tunakuwezesha’, katika
hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao Ilala jijini Dar Es Salaam jana.
Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa Airtel waliohudhuria hafla hiyo.
Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (pili kushoto), akimkabidhi
kijana Diana Mosha, msaada wa vifaa mbali mbali vya kutengenezea keki
kupitia mpango wa Airtel ‘FURSA Tunakuwezesha’, katika hafla fupi
iliyofanyika nyumbani kwao Ilala jijini Dar Es Salaam jana.
Wanaoshuhudia ni (kulia) ni Meneja mauzo wa Airtel Dar Es Salaam ,James
Moillo na wafanyakazi wengine wa Airtel.
Kijana
Diana Mosha (kushoto), akifafanua jambo baada ya kukabidhiwa msaada wa
vifaa mbali mbali vya kutengenezea keki kupitia mpango wa Airtel ‘FURSA
Tunakuwezesha’, kwa meneja masoko kanda ya Dar Es Salaam James Moillo
(pili kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao Ilala, Dar
Es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni meneja masoko wa Airtel kanda ya
Mbagala, Saleh Safi akifuatiwa na meneja wa huduma kwa Jamii wa Airtel,
Hawa Bayumi. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
*******************
KUFUATIA
uzinduzi wa hivi karibuni wa Airtel FURSA msimu wa mbili, Airtel
inaendelea kugusa maisha ya vijana nchini Tanzania na kuwawezesha
kufikia matarajio yao ya ujasiriamali. Leo Airtel FURSA imemfikia kijana
Diana Moshi, mwenye umri wa miaka 22 anayejihusisha na upikaji wa keki
jijini Dar Es Salaam.
Diana
amepokea ruzuku katika mfumo wa vifaa vya kufanyia kazi vikiwemo trei
za keki, mashine za kuchanganyia unga wa keki, mashine za kupambia keki,
jokofu na jiko la gesi .Mbali na vifaa hivyo Diana atapokea mafunzo
maalum ya ujasiriamali na ushauri wa biashara ya keki kutoka kwa mtaalam
maalum na maarufu wa biashara ya keki hapa jijini.
Kutoka
alipoanzia akiwa na mtaji mdogo sana wa kuanzia biashara, Diana
aliendelea kuwa makini na kutilia mkazo wa ndoto yake. Pamoja na ukosefu
wa vifaa Diana hakukata tamaa bali alijifunza kupitia kwa jirani na
kukodisha vifaa vya kufanyia kazi kutoka kwa wafanyabiashara wengine.
Akiwa na furaha kubwa alisema; "Niliona Airtel FURSA kama fursa ambayo
inaweza kusaidia kupunguza mapambano na kuongeza matumaini yainua
biashara yangu, ninashukuru kwamba leo Airtel FURSA imenifikia na kuweza
kubadilisha maisha yangu. Nimeanza nikiwa na mtaji mdogo sana lakini
leo Airtel imenidhihirishia kwamba kufanya kazi kwa bidii na uvumilivu
inaweza kutimiza ndoto yako ".
Diana
aliahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa vile yeye sasa anauwezo
kwa kuwa na zana madhubuti za kuzalisha zaidi. "Ninaamini katika kipindi
cha muda mfupi nitaweza kuzalisha zaidi na kuajiri wengine ili kusaidia
biashara yangu. Mimi ni shuhuda wa kweli kabisa wa walengwa wa Airtel
FURSA walioomba na kupata msaada . Ninaahadi kusaidia jamii yangu
inayonizunguka kwa sababu ninaelewa fika ni jinsi gani vijana wenzangu
wanavyopata tabu huko mtaani na sitaacha kuendelea kuwahamasisha. "
Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa
Bayumi
alimpongeza Diana kwa kufwata ndoto zake na kuhimiza vijana wengine
kuiga mfano wa Diana. Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano Bi
Bayumi alisema "Diana ametutia nguvu na kuweza kushiriki sehemu ya
safari ya ndoto zake kwani ameanza akiwa hana kitu , si kwa mtaji tu
lakini hata uzoefu wa kufanya biashara hii. Lakini leo hii ameweza kuuza
keki kupitia mitandao na kujipatia hela. Tunaamini vifaa tunavyompatia
Diana leo vitabadilisha maisha yake na kuinua biashara yake na kuongeza
wateja wengi zaidi.
Tunawahimiza
vijana wengi hapa nchini kuchangamkia Airtel FURSA si tu inayotolewa
kwa vitendea kazi bali na elimu ya biashara ambayo imekuwa ikitolewa
nchi nzima hapa Tanzania, pia kwa kupata maelekezo ya biashara kupitia
mitandao yetu ya kijamii inayosadia kuelekeza vijana jinsi ya kukuza
biashara zao, kujenga fursa kwa ajili ya wengine na kuwa na huduma na
jami zao zinazowazunguka.
Airtel,
kwa mara nyingine tena katika mpango wake wa Airtel FURSA umeahidi
kuendelea kugusa maisha ya wa Tanzania kwa kuwawezesha vijana kupitia
Airtel FURSA. Hadi sasa Airtel imeweza kufikia vijana zaidi ya 2,500
nchini Tanzania na na imeahidi kufikia vijana zaidi ya 1500 katika
kipindi cha miezi sita ijayo.
0 comments:
Post a Comment