Aina
mpya ya rangi ambayo imeundwa kwa mtindo maalum ili kurejesha mkojo kwa
anayejaribu kuukojolea ukuta uliopakwa rangi hiyo, imeanza kujaribiwa na
manispaa moja jijini London.
Rangi
hiyo ya majimaji itakuwa ikipakwa katika maeneo maarufu kwa wanywaji pombe,
katika tarafa za Shoreditch na Dalston, mashariki mwa London.
Manispaa
ya Hackney, imesema imekuwa ikitumia £100,000 kusafisha mkojo kutoka katika
kuta za manispaa hiyo na pembezoni mwa barabara, mahala ambapo watu huenda haja
ndogo ovyo.
Feryal
Dermici, ambaye ni mbunge wa manispaa hiyo anasema: "ikiwa hatua ya
kuwapiga faini haiwazuii kukojoa ovyo barabarani na pembezoni mwa njia, sasa
hatari ya kumwagikiwa na mkojo wao wenyewe, litakuwa jambo la busara".
Sasa,
adhabu ni kujenga kizuizi itakayopakwa rangi ambayo itawezesha mkojo kumrudia
mkojoaji, ili anapomwagikiwa na mkojo wake mwenyewe, basi atapata adhabu
inayomfaa.
Pia
lengo jingine ni kuzuia mkojo kulowesha ukuta, kuondoa madoadoa ya uchafu na
uvundo.
Haijafichuliwa
hasa maeneo ambayo itapakwa rangi hiyo, ili wanaoenda haja wasijue na kukwepa
maeneo hayo pekee. Source:BBC
0 comments:
Post a Comment