Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli,
amemtmia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC)
Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu Mstaafu Plasdus
Gervas Nkalanga (OSB) akiwa na umri wa miaka 96 kilichotokea Ijumaa tarehe
18 Desemba, 2015 katika hospitali ya Mtakatifu Joseph Peramiho, Wilaya ya
Songea Mkoani Ruvuma.
Mhashamu Askofu Nkalanga aliyekua Askofu wa Jimbo la Bukoba alistaafu
uaskofu mwaka 1974 na kujiunga na watawa wabenediktini wamonaki ambapo
aliamua kwenda kuishi katika Abasia ya Hanga iliyopo katika Wilaya ya
Namtumbo Mkoani Ruvuma alikofunga nadhili za milele Mwaka 2009
Katika salamu zake Rais Magufuli amesema Askofu Nkalanga
atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kuhimiza imani na uchapakazi
kazi katika kipindi chote cha miaka 54 ya uaskofu wake na utawa wake akiwa
katika Abasia ya Hanga.
Amesema Marehemu Askofu Nkalanga ambaye baada ya kustaafu aliamua
kuingia katika utawa akianzia katika ngazi ya chini kabisa ya Unovisi hadi
alipofunga nadhili za milele za utawa, ameacha mfano mzuri unaohimiza
jamii kuishi kwa upendo, unyenyekevu na kutokata tamaa.
"Kupitia kwako Baba Askofu Ngalalekumtwa napenda kuwapa pole
nyingi Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Abate wa Abasia ya
Hanga, watawa na waumini wote wa kanisa Katoliki kwa kupoteza mtu muhimu
aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kanisa na jamii kwa
ujumla" amesema Rais Magufuli
Rais John Pombe Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya
Marehemu Askofu Nkalanga mahali pema peponi, Amina.
Gerson Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
20
Desemba, 2015
0 comments:
Post a Comment