Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga akishiriki kufanya usafi katika maeneo ya kuzunguka ofisi za LAPF Dodoma pamoja na kituo cha Afya Makole.
Baadhi ya Watumishi wa LAPF walioshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika kituo cha Afya Makole Dodoma Mjini katika kuadhimisha siku ya Uhuru.
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga akizungumza jambo kabla ya kabidhi Msaada wa Mashuka na Vyandarua kwa ajili ya kituo cha Afya Makole kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Dr. Jasmine Tisekwa.
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga akikabidhi Msaada wa Mashuka na Vyandarua kwa ajili ya kituo cha Afya Makole kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Dr. Jasmine Tisekwa.
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga akikabidhi Msaada wa vyandalua kwa ajili ya kituo cha Afya Makole kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Dr. Jasmine Tisekwa.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akitoa neno la shukurani kwa niaba ya uongozi wa kituo cha Afya Makole baada ya kupokea masaada.
Mfuko
wa Pensheni wa LAPF wenye makao yake makuu mjini Dodoma, umetoa msaada
wenye thamani ya shilingi 2,800,000/= kwa kituo cha Afya cha Makole.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni Mashuka 50, Vyandarua 50 pamoja na
Vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi kwenye kituo hicho.
Msaada
huo umelenga kuboresha huduma kwa wagonjwa wanaolazwa kituoni hapo
wengi wao wakiwa ni kina mama wajawazito na watoto. LAPF inaunga mkono
jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za Afya nchini.
Kadhalika
katika kuadhimisha siku ya Uhuru tarehe 9 Disemba na kuunga mkono agizo
la mheshimiwa Raisi Dk. John Pombe Magufuli la kufanya usafi katika
kuadhimisha siku hiyo watumishi wa LAPF wakiongozwa na Mkurugenzi mkuu
Bw. Eliud Sanga wameshiriki kufanya usafi katika maeneo yote ya nje na
ndani ya kituo hicho cha Afya cha Makole.
Mfuko
wa Pensheni wa LAPF umekuwa ukitoa misaada mbali mbali ya kijamii
nchini katika kuboresha huduma za kijamii kama elimu, maji, michezo,
vituo vya kulea watoto yatima na afya. Katika sekta ya afya LAPF imekuwa
ikitoa vifaa mbali mbali kama vitanda vya wagonjwa, vitanda vya
kujifungulia, dawa, mashuka, vyandarua pamoja kufanya ukarabati katika
baadhi ya vituo vya afya kila bajeti ya misaada kwa jamii inaporuhusu.
LAPF
inaamini kuwa misaada hii inawasaidia wanachama wake pamoja na
watanzania wote kwa ujumla, pia inawaasa wadau wengine nchini kuchangia
huduma mbali mbali za kijamii ili kuboresha maisha ya watanzania na
hatimaye kuleta usawa katika jamii.
STAAFU KWA UFAHARI NA LAPF.
0 comments:
Post a Comment