Nafasi Ya Matangazo

December 08, 2015

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Khamisi Mwinyimvua akikabidhi tuzo ya mshindi wa tatu ya Muwasilishaji bora wa hesabu za benki iliyokwenda kwa Benki ya DCB na kupokelewa na Mkurugenzi wa fedha na Mipango wa DCB Bank, Consolatha lalika, Dar es Salaam juzi. Tuzo hizo Tuzo na Uwasilishaji Bora wa Hesabu kwa mwaka 2014, kwa Taasisi za Umma na Binafsi na kuandaliwa na Boadi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).

Mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Hamisi Mwinyimvua (kulia) akizungumza katika hafla ya kutoa tuzo kwa makampuni na taasisi zilizofanya vizuri katika ukaguzi wa taarifa za fedha kwa makampuni na idara anuai nchini katika shindano la ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014. Jumla ya makampuni na taasisi 58 zilishiriki katika kinyang'anyiro hicho cha ukaguzi wa taarifa za fedha kwa hiyari.
Posted by MROKI On Tuesday, December 08, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo