Meneja wa bia ya Castle LITE nchini,Victoria Kimaro
akitambulisha nembo mpya ya bia hiyo ikiwa baridi wakati hafla ya uzinduzi wake
kwenye hafla iliyofanyika kwenye baa ya Break Point-Kinondoni jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wageni waliohudhuria
hafla uzinduzi wa nembo mpya ya Castle LITE inayobadilika rangi na kuwa bluu
inapokuwa kwenye ubaridi sahihi mpya ya kinywaji hicho wakipatiwa maelezo juu ya mabadiliko hayo ya
nembo .Hafla hiyo ilifanyika kwenye baa ya Break Point –Kinondoni jijini Dar es
Salaam jana na kuhudhuriwa na wananchi kutoka sehemu mbalimbali za jiji
Meneja wa bia ya Castle LITE ,Victoria Kimaro akiongea na waandishi wa
habari wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa nembo.
Baadhi ya wateja waliofika
kwenye hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya bia ya Castle LITE inayobadilika
rangi na kuwa bluu inapokuwa kwenye ubaridi sahihi wakishindana kuweka mikono kwenye barafu
wakiangaliwa na Meneja wa bia ya Castle LITE Tanzania ,Victoria Kimaro (kulia)
wakati wa hafla ya uzinduzi na nembo hiyo ambapo ulikuwepo na michezo
mbalimbali ya burudani iliyowawezesha washindi kujinyakulia zawadi mbalimbali.
Baadhi ya maofisa wa Kampuni
ya Bia Tanzania ( TBL) Kutoka kushoto ni Gareth Jones na Aidan Thomas wakishindana kuweka mikono kwenye barafu
wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya bia ya Castle LITE. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika kwenye baa
ya Break Point –Kinondoni jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na wananchi
kutoka sehemu mbalimbali za jiji. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.
Uzinduzi wa nembo hii yenye kuleta burudani ulifanyika
mwishoni mwa wiki katika baa ya Break Point-Kinondoni na kuambatana na burudani
na mashindano ambayo yaliwawezesha washindi kujinyakulia zawadi mbalimbali
kutoka kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Meneja wa Castle Lite,Victoria
Kimaro alisema kuwa ubunifu huu ni wa aina yake na wa kwanza kufanyika nchini
na lengo kubwa ni kuwapatia watumiaji wa kinywaji hiki burudani ya ziada wanapokitumia kikiwa na kiwango cha ubaridi unaostahili.
“Pale nembo yenye hekalu
inayopatikana kwenye chupa ya Castle Lite mpya inapobadilika na kuwabluu,itaonyesha kwamba bia ya
Castle LITE imapata ubaridi zaidi na kukufanya uburudike na kufurahiazaidi.Ubunifu huu ni mpya
Tanzania na Afrika Mashariki na kutokana na ukanda huu kuwa wa joto,nembo hii
mpya itasaidia kumwonyesha mnywaji bia
gani ina ubaridi zaidi”Alisema.
Wateja mbalimbali
waliohudhuria uzinduzi huo na kuonja Castle Lite katika ubaridi unaostahili walisema
kuwa nembo mpya itawasaidia kutambua ubaridi
wa kinywaji tofauti na ilivyokuwa hapo awali “Ubunifu huu ni wa aina yake kwa
kuwa unatuwezesha kutambua ubaridi unaostahili wa bia wa kutazama nembo tofauti
na ilivyokuwa hapo awali”Alisema Amandus Njau Mkazi wa Kinondoni mmoja wa
wananchi waliohudhurua hafla hiyo.
0 comments:
Post a Comment