Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya Posta Tanzania, TPB, Henry Bwogi, akizibua chemba ya kupitisha maji
taka kwenye zoni 3 ya soko la samaki la kimataifa Feri jijini Dar es Salaam
Desemba 9, 2015. TPB imeungana na watanzania katika kuunga mkono agizo la Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwataka wananchi kusherehekea sikukuu ya
Uhuru wa Tanganyika kwa kufanya usafi ili kutekeleza zana ya “Uhuru ni Kazi”
badala ya kufanya sherehe na matamasha huku nchi ikakabiliwa na ugonjwa wa
Kipindupindu
Mfanyakazi wa TPB, akizibua chemba katika kutekeleza zana
ya Uhuru ni Kazi
Na K-Vis Media/Khalfan Said)
KATIKA kuunga mkono maelekezo
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa wananchi na taasisi za serikali
kufanya usafi siku ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika, Benki ya
Posta Tanzania, TPB, nayo iliungana na wananchi hususan eneo la soko la
kimataifa la samaki Feri, katika kutekeleza agizo hilo.
Wakati Mh. Rais alishirikiana
na majirani zake, wavuvi na wachuuzi wa samaki pale nje kidogo ya uzio wa
Ikulu, hali ilikuwa hivyo hivyo kwenye maeneo mengi, ya nchi ambapo katika eneo
hilo la soko la Feri, TPB walipewa eneo la kufanyia usafi kwenye zoni namba 1
na eneo la kuegeshea mitumbwi maarufu kama “Lebanon” ambapo Kaimu Afisa
Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Henri Bwogi, aliwaongoza wafanyakazi wa benki
hiyo katika kufagia, kuzibua mitaro na chemba za maji taka, hali kadhalika
kupakia taka kwenye malori ya kubebea taka.
Katika hatua nyingine Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw. Bwogi, alikabidhi vifaa vya kufanyia
uasafi viliovyokuwa vikitumiwa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa uongozi wa soko
ili waendelee na kazi ya usafi siku za usoni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, aliagiza sherehe za mwaka huu za
Uhuru wa Tanganyika, zisherehekewe kwa kufanya kazi ili kutekeleza zana ya
“Uhuru ni Kazi” badala ya kufanya matamasha na shamra shamra kwenye viwanja
mbaklimbali nchini.
“ Nimefurahishwa sana na
wananchi jinsi walivyojitokeza kwa wingi kwenye maeneo mbaklimbali ya nchi
katika kufanya usafi ili kuiweka nchi yetu safi na kujikinga na maradhi kama
Kipindupindu.” Rais Magufukli aliwaambia majirani zake baada ya zoezi la
kufanya usafi.
Naye Kaimu Afisa Myendaji Mkuu
wa TPB, Bw. Bwogi, alisema TPB kama taasisi ya serikali iliamuru wafanyakazi
wake, wafike kazini na kushiriki katika kufanya usafi na sisi tumeona tuje
kuungana na wenzetu wa feri ili kutekeleza maelekezo ya Rais wetu.” Alisema.
0 comments:
Post a Comment