Meneja Uhusiano wa Airtel
Bwana Jackson Mmbando akionyesha huduma mpya ya "Airtel TV" inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa huduma
hiyo itakayowawezesha
wateja wa Airtel kuangalia vipindi katika vituo mbalimbali vya television
kupitia simu zao za mkononi, akishuhudia ni Meneja huduma za ziada wa Airtel,Prisca Tembo.
Meneja Uhusiano wa Airtel
Bwana Jackson Mmbando akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya
"Airtel TV" itakayowawezesha wateja wa Airtel kuangalia vipindi
katika vituo mbalimbali vya television
kupitia simu zao za mkononi.
***********
*
Kuunganishwa na chanel 8 za ndani na nje
* Kujiunga
na vifurushi vya kuangalia TV bila kikomo vya siku, wiki na mwezi
Dar es Salaam, Tanzania 19
Novemba 2015, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua huduma ya
ziada itakayowawezesha wateja wake nchi nzima kuangalia vipindi vya
televisheni katika vituo vya ndani na nje ya nchi kupitia simu zao za
mkononi.
Huduma hii mpya ijulikanayo
kama "Airtel TV" imeunganishwa na vituo 8 za televisheni vya ndani na
nje ya nchi na kuwawezesha wateja wa Airtel kuangalia vipindi vilivyopita
katika tamsilia wanazozipenda,
kuangalia sinema na video
wanazohitaji kupitia simu zao.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa
"Airtel TV" Meneja Uhusiano wa Airtel , Bw Jackson Mmbando alisema
"kwa kawaida mara nyingi watanzania wanaangalia vipindi vya televisheni
wakiwa nyumbani wakati wa jioni baada ya kutoka katika kazi zao.
Tunazindua huduma yenye gharama nafuu itakayowawezesha wateja wetu kupata
taarifa pindi wasipokuwapo majumbani mwao.
"Airtel TV"
itawapatia uzoefu wa kipekee na kuwahabarisha wateja wetu wakati wowote
wakiwa katika shughuli zao au kwenye foleni, bila kikomo kupitia
simu zao za mkononi" " huduma hiii imelenga kukidhi mahitaji ya
wateja kwa kuwapatia habari kiurahisi kwa kujiunga na kifurushi cha siku , wiki
au mwezi.
Tunaamini huduma hii
itapunguza uwiano wa watu wasiokuwa na fursa ya kuangalia Televishoni na pia
kuwawezesha kupata matukio kwa wakati kupitia simu zao mahali popote pale
walipo" aliongeza Mmbando Akiongea kuhusu mahudhui na jinsi ya kujiunga na
huduma hiyo, Meneja huduma za ziada ,Prisca Tembo alieleza zaidi kuhusu
dhamira yao ya kutoa huduma yenye kiwango cha juu na gharama nafuu. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
" tunayo
furaha kuwawezesha watanzania kuangalia vipindi vya televisheni kupitia
simu zao kwani tunaenda sambamba na mpango wa serikali wa kidigitali wenye lengo
la kuwa na jamii kupata taarifa za yanayotokea ndani na nje ya nchi kwa
wakati na kiwango cha juu.
Tembo aliongeza kwa kusema ili
kupata huduma ya "Airtel TV" mteja anatakiwa kupakua au
kudownload application kwa kupitia linki ya https://goo.gl/iSvaJC kwa
simu za Android na https://goo.gl/IMvzCt kwa simu za IOS.
Baada ya kuzi download mteja
ataweza kununua kifurushi cha internet maalum cha Televisheni kwa kupiga
*148*88# tozo za kujiunga ni Tshs 499 kwa siku, Tshs 2,999 kwa wiki
naTshs 11,999 kwa mwezi. Vituo vinavyopatikana katika "Airtel TV" ni
pamoja na Star TV, TBC, Fight Box, 360 tune box, Citizen, FilmBox, Channel Ten
na Aljazeera.
0 comments:
Post a Comment