Na Father Kidevu Blog
Rais John Magufuli amesitisha maadhimisho ya siku ya Ukimwi kitaifa ambayo yalikuwa yafunguliwe mkoani Singida leo na kufikia kilele chake Desemba mosi mwaka huu mjini humo.
Rais John Magufuli amesitisha maadhimisho ya siku ya Ukimwi kitaifa ambayo yalikuwa yafunguliwe mkoani Singida leo na kufikia kilele chake Desemba mosi mwaka huu mjini humo.
Badala yake Rais Dk Magufuli ameagiza fedha zote
ambazo zilitengwa na serikali pamoja na wahisani mbalimbali kwaajili ya
maadhimisho hayo zielekezwe kununua dawa kwaajili ya waathirika wa Ukimwi na vitendanishi.
Akizungumza na moja kwa moja na Televisheni ya
Taifa (TBC), Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi
(TACAIDS), Dk Fatma Mrisho, alisema serikali imeagiza jana wakati tayari mkuu
wa Mkoa wa Singida akiwa ameshafungua maonesho ya maadhimisho hayo.
“Serikali imesitisha maadhimisho ya mwaka huu
Singida na badalayake fedha zilizopangwa kwaajili ya maadhimisho ziende
zikanunue dawa za virusi vya Ukimwi, dawa za kudhibiti maambukizi ya ukimwi na
vitenganishi,” alisema Mrisho.
Dk Mrisho alisema kuwa tayari taarifa za kusitisha maadhimisho hayo zimesha wafikia washiriki na wale walio kuwa njia kuelekea Singida wamegeuza. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
Katika maadhimisho ya mwaka huu serikali ilitenga
kiasi cha shilingi Milioni 18 kwaajili
ya maadhimisho hayo huku kila mshiriki katika maonesho hayo akiachangia kiasi
cha sh laki tano.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
Dar es Salaam jana, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi
(TACAIDS), Dk Fatma Mrisho alisema maadhimisho ya mwaka huu yakuwa yatanguliwe na
maonesho ya wadau yatakayojumuisha huduma mbalimbali zikiwamo za utoaji elimu
na burudani.
Dk Mrisho
alisema huduma nyingine zilizopangwa kutolewa katika maadhimisho hayo ya wiki
moja ni upimaji wa hiari wa watu zaidi ya 3,500
wanaoishi na virusi vya Ukimwi na utoaji ushauri nasaha, upimaji wa
shingo ya uzazi, sukari, uzito, damu na kupata elimu itakayotolewa kupitia
vikundi vya sanaa na burudani.
Maadhimisho ya mwaka huu yanachagizwa na kaulimbiu
ya ‘Tanzania bila maambukizi mapya ya VVU, vifo vitokanavyo na Ukimwi na
ubaguzi na unyanyapaa inazewekana.’
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone
aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni kuwa maadhimisho
hayo yanatarajiwa kuanza Novemba 24 mwaka huu kwenye viwanja vya Peoples Club
ambapo uzinduzi utakuwa Novemba 25 kabla ya kilele, Desemba mosi.
Hii ni mara ya tatu tangu Rais Dk Magufuli aingie
madarakani kuzuia maadhimisho yanayogharimu fedha nyingi na sherehe na fedha
zake kuelekeza ikanunulie vifaa tiba mahospitalini.
Awali Rais aliagiza fedha zilizotengwa kwaajili ya
hafla ya uzinduzi wa Bunge zaidi ya shilingi Milioni 225 ziende kununulia
vitanda vya hospitali ya taifa Muhimbili.
Aidha Rais pia alisitisha maadhimisho ya siku ya
Uhuru Desemba tisa mwaka huu na badala yake watu wafanye kazi katika maeneo yao
ya kazi hasa usafi wa mazingira.
0 comments:
Post a Comment