Nafasi Ya Matangazo

October 16, 2015

Maafisa wa Polisi na wataalam wakichunguza mabaki ya chopa 5Y-DKK aliyokuwa akisafiria Mgombea Ubunge wa Ludewa na kupata ajali eneo la Hifadhi ya Selous, Kilombero mkoani Morogoro jana.Picha: Francis Godwin
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa na Mgombea pekee wa jimbo hilo katika uchaguzi unaotaraji kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, Deo Haule Filikunjombe (43) amefariki dunia kwa ajali ya chopa.

Mbali na Filikunjombe pia watu wengine wa tatu waliotambulika kuwa ni Rubani wa Helkopta hiyo, Capt. Willium Silaa, Kasablanka Haule na Egid Mkwela wamaefariki katika ajali ya chopa iliyotokea jana jioni katika hifadhi ya Selous Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. 

Rubani wa HelkoptaAS-35 iliyokuwa na usajili 5Y-DKK mali ya kampuni ya General Aviation Service ya jijini Dar es Salaam ambaye ni baba wa aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilala na Mgombea Ubunge wa jimbo la Ukonga Jerry Silaa. 

Jerry Silaa amethibitisha kutokea kwa kifo cha baba yake ambapo pia Kamanda wa Operation wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuthibisha vifo hivyo vya watu wanne.


Filikunjombe pamoja na wenzake hao walikuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Ludewa. 
  
Deo Filikunjombe anakuwa ni mgombea wa 6 kufariki tangu akuanza kwa Kampeni za Uchaguzi mwaka 2015 ambapo uchaguzi wake unataraji kufanyika Oktoba 25 mwaka .  

Wagombea hao ni Mohamed Mtoi wa CHADEMA jimbo la Lushoto,  Celine Kombani wa CCM jimbo la Ulanga Mashariki, Estomih Malla wa Chama cha ACT-Wazalendo Mgombea Ubunge jimbo la Arusha Mjini, Dk Abdallah Kigoda wa CCM Jimbo la Handeni Mjini na, Dk Emmanuel Makaidi wa NLD jimbo la Masasi aliyefariki jana Oktoba 15, 2015.
Hii ndio Chopa 5Y-DKK aliyokuwa akiitumia Deo Filikunjombe katika kampeni zake.
 
Capt. Willium Silaa enzi za uhai wake. 
Posted by MROKI On Friday, October 16, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo