Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Sabasaba Moshingi(wapili kulia), akihudumia wateja kwenye tawi la benki hiyo Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa Oktoba 16, 2015, kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo.
**************
NA
K-VIS MEDIA
KATIKA
kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake hapa nchini, Benki ya Posta
Tanzania, imeweka mashine maalum ambayo wateja wa benki hiyo wanaofika kupatiwa
huduma watatoa maoni yao juu ya huduma wazipatazo kwa kubonyeza vitufe
vinavyoelekeza nini maoni yake juu ya huduma aliyoipata.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa
wateja ya benki hiyo, kwenye tawi lake la Kijitonyama jijini Dar es Salaam,
Oktoba 16, 2015, Aisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi alisema,
benki yake imelenga kutoa huduma zilizo bora na za kisasa ili kurahisisha
utendaji wake wa kazi.
Moshingi ambaye aliongoza
maafisa wa benki hyo kutoka makao makuu kwa kutoa huduma kwa wateja,
kuwasikiliza na kuwasaidia namna ya kujaza fomu na kutoa pesa, alisema,hatua ya
yeye kuongoza maafisa wake kutoa huduma, ni kuwaonyesha wateja kuwa benki yao inawajali.
“Ili kufanikisha lengo hili
benki imeanzisha matumizi ya mashine za kisasa zitakazomuwezesha mteja kutoa
maoni ya jinsi gani anafurahia au kutofurahia huduma zetu bila kuhitaji
kuandika kwenye karatas, mteja atabofya kitufe ili kupata maoni yake, nasi
tutayafanyia kazi maoni yake haraka iwezekanavyo.”i.” Alisema Moshingi.
Alisema matumizi ya mashine
hizo yataboresha utoaji huduma za kibenki, na hivi sasa mipango ya kuziweka
kwenye kila tawi inaendelea.
Moshingi akimuelekeza mteja namna ya kujaza fomu za kuweka pesa
Afisa wa operesheni wa TPB tawi la Kijitonyama, Agatha Ngoile, (kushoto), akimuhudumia mteja
Mteja akibonyeza kitufe kutoa maoni yake baada ya kupata huduma
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, akibadilishana mawazo na Meneja wa shirika anayeshughulikia mawasiliano, Norvis Moses
Moshingi, (wapili kushoto), akizungumza na Norvis, huku Meneja wa tawi la TPB, Kijitonyama, Emmanuel Kimola akiteta jambo na Afisa Habari Theo Mwakifulefule
Meneja Masoko wa TPB, Deo Kwiyukwa, (kushoto), Meneja Biashara, Frank Mushi, (katikati), na Afisa Masoko, Grace Majige, wakibadilishana mawazo
Agatha akiwa kazini
Moshingi akiwa anahudumia mteja kwenye teller
0 comments:
Post a Comment