Na Woinde Shizza,Arusha
Kuelekea
uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 25 mwaka huu Serikali imetakiwa kukabiliana
na viashiria vya uvunjifu wa amani na kuvipatia ufumbuzi ili kuhakikisha uchaguzi
huru na wa haki utakaodumisha amani ya taifa.
Hayo
yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Apet Jijini Arusha Peter Aham katika mjadala wa masuala ya amani hasa katika
kipindi cha uchaguzi ulioudhuriwa na Wawakilishi kutoka tume ya uchaguzi,Jeshi
la Polisi,Vyama vya Siasa pamoja na wadau wa amani.
Peter Ahham
amesema kumekua na dalili za wazi za baadhi ya mamlaka kuonekana kuegemea
upande mmoja ikiwemo Tume ya Uchaguzi,Jeshi la Polisi na baadhi ya Vyombo vya
habari jambo ambalo linapingana na taaluma na weledi na linaweza kuathiri amani.
Mkuu wa
wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu amesema kuwa kwa muda mrefu amani iliyodumu
nchini imekua ikihatarishwa na masuala ya udini,ukabila na itikadi za kisiasa
hivyo kila mtanzania anajukumu la kulinda amani katika kipindi hiki cha
uchaguzi
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la Kiserikali la USIP ,Dr.James Jesse
pamoja na Kamishna wa Polisi mkoa wa Arusha Edward Balele amesema kuwa kila
mtanzania,vyama vya siasa vinawajibu wa kulinda amani na kuhakikisha kuwa
uchaguzi unakua huru na salama
Siku chache zimesalia kufikia Octoba
25 ambapo uchaguzi mkuu wa kitaifa unatarajia kufanyika ambapo Watanzania watapata
viong ozi wapya kuanzia ngazi ya Urais ,Ubunge na Udiwani huku suala kubwa
linalogonga vichwa vya watu wengi ni juu ya uwepo wa haki na amani katika
uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment