Mgombea Udiwani Kata ya Mbagala Kuu, Yusuf Manji akiwa ameshikana mikono na Mgombea wa ubunge wa jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu kwenye uzinduzi wa mikutano ya kampeni zake.
Mgombea ubunge jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu
akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika viwanja vya Chamazi
Shule.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Shamsi Vuai Nahodha akimnadi
mgombea ubunge jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu (kushoto) wakati wa uzinduzi
wa kampeni zake katika viwanja vya Chamazi Shule.
Wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za
mgombea wa ubunge wa Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu.
Mgombea wa
Ubunge katika jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa
Mangungu (kushoto) akitambulisha wagombea wa udiwani wa kata za
jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, kwenye uzinduzi wa mikutano ya kampeni zake.
***********
Alisema kuna tatizo la kutokuwa na Shule za Sekondari haswa za kuanzia kidato cha tano, hivyo watajipanga kuongeza madarasa na kujenda shule nyingine za Sekondari."Kwenye sehemu ya shule za Sekondari tutaongeza majengo ya madarasa ili wanafunzi wakaofanya vizuri wapate nafasi ya kuendelea na kuna kata nyingine tutajenga shule za Sekondari"alisema Mangungu.
John Magufuli na kuchagua madiwani wa CCM, ili waweze kuwa kitu kimoja na kuweza kushirikiana katika kuwaletea maendeo.
Nahodha alisema ana amini wakimchagua mbunge, Rais na madiwani wa CCM wataweza kufanikisha ahadi zao.
Na Mwandishi Wetu
MGOMBEA wa Ubunge wa tiketi
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo jipya la Mbagala Issa nangungu, amesema endapo atachaguliwa
kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha vijana wanapewa kipaumbele
katika kupata ajira.
Mangungu aliyasema hayo juzi
wakati wa uzinduzi rasm wa kampeni zake katika jimbo hilo, zilizofanyika kwenye
viwanja vya Chamazi Shule Jijini Dar es Salaam, kuwa atahakikisha suala la
ufundi kwa vijana linapewa kipaumbele.
Alisema katika
kuhakikisha vijana wanapata ajira ataishawishi Serikali kufungua tawi la Chuo
cha Ufundi (VETA), katika Jimbo hilo ili vijana waweze kusoma na kupata
kazi. "Nitahakikisha
napigania uanzishwaji wa tawi la Veta katika la Mbagala hili vijana waweze
kupata mafunzo ya ajira"alisema Mangungu. Katika hatua nyingine Mangungu
alisema kuna tatizo la shule katika baadhi ya kata atahakikisha wanajenga shule
ili kuepusha wanafunzi kutembea kwa muda mrefu kupata elimu.
Alisema kuna tatizo la kutokuwa na Shule za Sekondari haswa za kuanzia kidato cha tano, hivyo watajipanga kuongeza madarasa na kujenda shule nyingine za Sekondari."Kwenye sehemu ya shule za Sekondari tutaongeza majengo ya madarasa ili wanafunzi wakaofanya vizuri wapate nafasi ya kuendelea na kuna kata nyingine tutajenga shule za Sekondari"alisema Mangungu.
Alisema kuwa katika upande
mwingine atahakikisha madereva wa bodaboda wanatambulika kwa sababu nao ni wapo
kwenye ajira.Mangungu alisema kuwa lazima madereva wa bodaboda wawe kwenye
ajira rasmi, hivyo kama mbunge atawatetea madereva hao.
Alisema kuna tatizo la Maji na
Barabara vipi ndani ya vipaumbele vyake ana amini akipata nafasi yeye na
madiwani wake wa CCM watafavifanyia kazi.
Mangungu amewataka wakazi wa
mbagala kumchagua yeye katika nafasi ya ubunge, ikiwa pamoja na kumchagua
mgombea wa Urais
John Magufuli na kuchagua madiwani wa CCM, ili waweze kuwa kitu kimoja na kuweza kushirikiana katika kuwaletea maendeo.
Katika mkutano huo wa ufunguzi
wa Kampeni ya za mbunge huyo, mgeni rasmi alikuwa Shamsi Vuai Nahodha ambaye ni
Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa (NEC), ambaye aliwataka wakazi wa jimbo hilo
wasifanye makosa kumchagua mbunge wa upinzani.
Nahodha alisema ana amini wakimchagua mbunge, Rais na madiwani wa CCM wataweza kufanikisha ahadi zao.
Alisema CCM ina ilani nzuri
inayotekelezeka kwa wananchi wake hivyo kuna kila sababu ya kulitambua hilo.
Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, amewataka wananchi wa jimbo hilo kutofanya
makosa ya kuwapata uongozi wa wa vyama vya upinzani, kwa sababu hawana sera,
hivyo watumie nafasi hiyo kuchagua wagombea wa CCM.
Madabida alisema kuwa siku ya
Oktoba 25, wahakikishe wanajitokeza kwa wingi kwenda kuwapiga kura na
kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika mkutano huo mgombea
Ubunge aliwatambulisha wagombea Udiwani wake katika Kata 10 zilizopo katika Jimbo
hilo akiwemo Yusuph Manji na Said Fella.
0 comments:
Post a Comment