Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ni
nahodha wa timu ya viongozi wa dini, Alhadi Mussa Salum, akinyanyua juu kikombe
cha ushindi wa pili baada ya kumalizika kwa pambano la soka kati ya viongozi
hao na mabalozi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo Oktoba 17, 2015. Mabalozi walishinda kwa mikwaju ya penati 3-2 na kutwaa kombe. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, na wakwanza ushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia,
anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo
NA
K-VIS MEDIA
KAMPUNI
ya Acacia imedhamini pambano la soka kati ya viongozi wa dini na mabalozi
wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania, pambano lililopigwa uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam jana Oktoba 17, 2015
Katika
pambano hilo, mabalozi waliibuka washindi kwa njia ya mikwaju ya penalty 3-2 na
kutwaa kombe.
Akitoa
nasaha zake kabla ya kuanza pambano hilo la kuenzi amani taifa linapoelekea
kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwezi huu, Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, aliwaambia washiriki kuwa, serikali
inaunga mkono jitihada za viongozi wa dini na mabalozi katika kuwaleta pamoja
wananchi hususan katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea kwenye uchaguzi.
Pambano
hilo la soka lililodumu kwa muda wa dakika 40, lilikuwa la utangulizi kabla ya
pambano la ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Yanga na Azam FC.
Akizungumza
mwishoni mwa mchezo huo, Meneja Mkuu wa Acacia anayeshugulikia a ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo, alisema, kampuni yake
imedhamini pambano hilo kwa kutambua umuhimu wa amani hapa nchini, ambapo
Acacia kama wawekezaji wanao wajibu wa kuunga mkono jitihada zozote za kijamii
katika kuhakikisha amani inakuwepo hapa nchini inakuwepo.
“Sote
tunatambua kuwa hivi karibuni taifa litaingiankwenye uchaguzi mkuu wa kuchagua
viongozi wetu, hivyo pambano hili la soka la viongozi wa dini na mabalozi
ambalo nia yake kubwa ni kuhamasisha amani miongoni mwa Watanzania katika
kipindi hiki cha uchaguzi limekuja wakati muafaka nasi kama Acacia tumeona
tuchangie katika jambo hili muhimui.” Alisema Assa.
Katika
pambano hilo lililofana, wachezaji wa timu zote mbili walionyesha ukakamavu wa
hali ya juu kwa kumudu kucheza kwa nguvu na umahiri mkubwa na kuwapa burudani
safi wapenzi wa soka.
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini, Filiberto Sebregondi, ambaye alikuwa nahodha wa timu ya soka ya
mabalozi, akinyanyua juu kombe baada ya timu yake kuishinda timu ya mabalozi
kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. Wanaoshuhudia
kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa
kampuni, Assa Mwaipopo, na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali, Alex Lugendo (wapili
kushoto)
Waziri Chikawe, (kushoto), akisalimiana na Assa Mwaipopo
"Ball Boys" wakiwa wamebeba bendera ya Acacia, wakati timu zikiingia uwanjani
Sheikh Alhadi akiwa kwenye mazoezi ya viungo na viongozi wenzake wa dini kabla ya mpambano huo
Sheikh Alhadi akifumua shuti
Mwamuzi wa pambano hilo Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akipuliza kipyenga
Sheikh Alhadi akijaribu kufunga penalty ambayo hata hivyo hakufanuikiwa kufunga
Timu ya viongozi wa dini iliyomenyana na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini
Timu ya soka ya mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa wanaowakilisha mashiorika na nchi zao hapa nchini
Waziri Chikawe, viongozi wa Acacia, na wale wa TFF wakisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili
Viongozi wa dini wakiongozwa na kocha wao wakati "wakipasha" kabla ya pambano hilo
Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo, akiwaeleza waandishi wa habari sababu za kampuni hiyo mudhamini pambano hilo la soka.“Sote tunatambua kuwa hivi karibuni taifa litaingiankwenye uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wetu, hivyo pambano hili la soka la viongozi wa dini na mabalozi ambalo nia yake kubwa ni kuhamasisha amani miongoni mwa Watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi limekuja wakati muafaka nasi kama Acacia tumeona tuchangie katika jambo hili muhimui.” Alisema Assa.
"Benchi la ufundi" la viongozi wa dini, kutoka kushoto, Sheikh Basaleh, Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, na Sheikh Othman, wakifuatilia kwa karibu pambano hilo
Nasaha za mgeni rasmi kwa timu zote mbili
Waziri Chikawe, (kulia), akiongozana na Assa Mwaipopo, (kushoto) na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex Lugendo, mara baada ya ukaguzi wa timu
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, (kushoto), ambaye alikuwa kamisaa wa mchezo aisalimiana na Assa Mwaipopo
Mazoezi ya viungo yakiendelea
0 comments:
Post a Comment