Nafasi Ya Matangazo

October 19, 2015

Kipande cha Video ya mahojiano
Kuelekea Shindano la Bongo Style  Competition , Ambalo linatarajiwa kufanyika Mwishoni mwa mwezi wa Kumi na moja mwaka huu, Majaji wamefanikiwa kuwapata washiriki ambao wataingia katika Kinyang'anyiro hicho

Akizungumzia Shindano hilo Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa alisema shindano hilo linalengo la kuibua vipaji vya vijana wenye kati ya umri wa miaka 18-25 katika nyanja za ubunifu mitindo na upigaji picha ili kuwahamasisha kutumia vipaji vyao kujiajili wenyewe. Aliongeza kuwa idadi ya Fomu zilizotumwa kwa njia ya mtandao zilikuwa 310 kati ya hizo zilizo pitiwa na Majaji pande zote ili kupata washiriki 20 zilikuwa fomu 285.

Aliwataja waliopita kushiriki katika upande wa picha ni pamoja na hao kwa upande wa  ni pamoja na Daniel Msirikale, Anneth Mgowano, Travis Gaudence, Victor Mpalile,Ebenezer Mmasi, Hassan Mohammed Ally, Rasheed Hamis, Erick Mwan'gonda, Nicetas Mtey na Nicetas Mtey

kwa upande wa Ubunifu wa mavazi na mitindo aliwataja washiriki hao ni pamoja na Anna Ben Paul,Eva Mary Sospeter,  Jocktan mwakeke
Lilian Ndanshau, Cecilia lyakulwa,Milly's Fenary Collection,Mamaland,Shahbaaz Sayed Yusuf,Salome Sebastian, na  Andrew Kalema

Nae Jaji wa Eneo la Mitindo Ambaye pia ni Balozi wa FASDO Martin Kadinda alizungumzia shindano hilo kuwa ni zuri na lipo kwa ajili ya kuibua vipaji vipya vya wanamitindo na kuongeza pia wale wote walioshiriki katika Shindano hili hasa walioleta fomu zao walikuwa wanauwezo lakini kwa kuwa ni shindano wachache ndio walikuwa wanatakiwa kulingana na vigezo na Masharti walivyoweka.

Akiongezea Jaji upande wa Picha Sameer Kermalli kwa niaba ya majaji wengine  amesema kuwa wamepokea na kupitia picha za washiriki wengi walioleta picha wamepitia na kugundua baadhi yao wamepiga picha nzuri ambazo zipo kitaalam na wengine wamepiga picha ka kuzi 'edit' sana jambo ambalo limesababisha kupunguza alama zao na pia wengine wametumia picha ambazo sio zao, pia aliongeza kwa kusema baadhi yao ambao wamechukuliwa pia wamefanya vizuri kutokana na ubunifu wao. 

Philipo Florian ambao wapo katika mitandao ya kijamii na waliokuwa wakipokea fomu hizo alisema kuwa fomu fomu nyingi zilikuja kwa kurudiwa rudiwa kitu ambacho kilichanganya kidogo mchanganuo, pia watu wengi  walipaa shida wakati wa kuweka Picha lakini hata hivyo wengi walifanikiwa na kushiriki kikamilifu. Pia Anna Semiono aliongeza kuwa zoezi lilienda kikamilifu na idadi ya wanawake na wanaume ambao walileta fomu zilikuwa sahihi ingawa baadhi yao walikosea kwa namna moja au nyengine kutokana na kuto elewa vizuri ni namna gani wangeweza wasilisha kazi zao, hata hivyo alisema changamoto hiyo haitakuwepo katika shindano lijalo kwa kuwa kutakuwa kuna elimu mbadala kupitia VIDEO CLIP itakayo onesha namna ya kutuma kazi zao.
Posted by MROKI On Monday, October 19, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo