Nafasi Ya Matangazo

September 22, 2015

Kamati ya Miss Tanzania inapenda kuwatangazia wadau wote wanaotaka kuandaa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 kutuma maombi yao ya uwakala kuanzia sasa hadi tarehe 30 Novemba 2015 ndio mwisho wa kupokea maombi ha yo.
 
Mashindano yatakayo fanyika ni ya mikoa tu, hakutakuwa na mashindano katika ngazi ya kitongoji, wilaya wala Kanda.
 
Sifa za kuwa Wakala wa Miss Tanzania ni pamoja na
 
1)      Uwe na Kampuni iliyosajiliwa na Mamlaka husika ya Serikali.
2)      Uwe na mtaji wa kutosha.
3)      Uwe na uwezo wa kuandaa shindano katika ufanisi mkubwa.
4)      Uwe mstari wa mbele katika kukuza sanaa za utamaduni nchini.
 
Wakala atakaye pitishwa na Kamati ya Miss Tanzania atapaswa kujisajili Baraza la Sanaa la Taifa.(BASATA) kabla hajapewa kibali cha kuandaa shindano.
 
Wilaya za Mkoa wa D’salaam, Ilala, Kinodoni na Temeke zitapewa hadhi ya Kimkoa, ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Elimu ya Juu.
 
Ada ya Uwakala ni shilingi milioni moja(1,000,000/-).
 
Ada ya Uwakala italipwa kwa Kamati ya Miss Tanzania baada ya maombi kukubaliwa na kupitishwa.
 
Maombi yatumwe kwa barue pepe   misstanzania2015@yahoo.com
Kwa mawasiliano na ufafanuzi zaidi piga namba zifuatazo:-
 
0673 521037  Katibu wa Kamati
0754 337043 Msemaji wa Kamati
0755 019288 Sekretariet.
 
Imetolewa na:
 
JUMA PINTO.
MWENYEKITI
KAMATI YA  MISS TANZANIA.
Posted by MROKI On Tuesday, September 22, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo