Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel
Tanzania, Hawa Bayumi (katikati), akiwakabidhi wawakilishi wa kikundi cha
MIRANACO mjini Mbeya vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia katika biashara yao ya
ufugaji wa nyuki. Kupitia mradi wa Airtel FURSA kikundi hicho kimewezeshwa kwa
kupatiwa mizinga ya nyuki, mashine za kukamulia asali, vifaa vya kinga ya nyuki
na zana zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki. Wakishuhudia kutoka
kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha FURSA Irine Paul akifuatiwa na Meneja mauzo
wa Airtel mkoani Mbeya Saidi Zani
************
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
imewawezesha vijana wajasiriamali wa kikundi cha MINARACO kutoka mkoani Mbeya
wanaojishughulisha na ufugaji wa nyuki.
Kikundi hicho kinaundwa na vijana 76 walioamua
kuungana na kujihusisha katika ufugaji wa nyuki ili kujikwamua na changamoto za
maisha. Kupitia mradi wa Airtel FURSA kikundi hicho kimewezeshwa kwa kupatiwa
mizinga ya nyuki 20, mashine za kukamulia asali 1, vifaa vya kinga ya nyuki 2,
chupa za lita 1, 400, chupa za asali za lita 5, 200 na zana zitumikazo
kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki
Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma kwa
jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema, “vitendea kazi waliopatiwa ni vyakisasa
zaidi na vitasaidia kuboresha ufugaji huo na kuwawezesha vijana hao kupata
mavuno zaidi ya waliokuwa wakipata awali”.
Akiongezea amesema, “mpango huo wa kuwawezesha
wajasiriamali vifaa ni sehemu ya mpango wa kampuni ya Airtel wa kuwawezesha
vijana ili kuboresha maisha yao na ya watu wanaowazunguka”.
“Sisi kama Kampuni ya mawasiliano tumeona ni
vizuri kushirikiana na wajasiriamali na hasa vijana wenye umri kati ya miaka
18-24 ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya biashara kwa
mafunzo na vifaa” alisema meneja huyo”.
Wakipokea msaada huo wameishukuru, Airtel kwa
kujitoa kwa kuwasaidia vijana katika kutatua changamoto zinazowakabili na
kuahidi kutumia vifaa hivyo kwaajili ya kuongeza uzalishaji ili kufikia malengo
waliojiwekea katika kikundi hicho.
“Hatukuamini kuwa Airtel itakuja kututembelea,
kuangalia mahitaji yetu na hasa kwa kutupatia msaada wa vifaa vya kisasa
walivyo tupatia leo, tunawashukuru sana na tunaahidi kutumia vyema msaada
huu ili kuhakikisha tunakuza na kuendeleza ufugaji bora wa nyuki” alisema
mwakilishi wa kikundi hicho John Maige.
Akiongezea Maige alisema, “Awali tulikuwa
na changamoto ya uchache wa mizinga, vifungashio vya asali na soko la uhakika,
lakini Airtel imetusaidia kwa kutupa mafunzo na vifaa vya kutosha vitakavyo
tusaidia kupata Asali ya kutosha na yenye ubora mzuri “.
Kampuni ya simu ya Airtel inazunguka nchi nzima
kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa
uwezeshaji kwa vijana.
0 comments:
Post a Comment