Mkuu wa Wilaya ya
Mbeya Nyiremba Munasa akizungumza na viongozi na wajumbe wa Tuiko Mkoa
wa Mbeya wakati akifungua mkutano ambao unalengo la kufanya uchaguzi kwa
kuwapata viongozi wapya wa Tuiko ngazi ya mkoa katika ukumbi wa chuo
cha wafanyakazi (OTU)Kabwe jijini Mbeya .(Picha Jamiimojablog)
Katibu wa Tuiko Mkoa wa Mbeya Ndugu Merbota Kapinga akizungumza katika mkutano huo
Mwenyekiti wa
Tuiko Mkoaa wa Mbeya Daudi Mpolya akizungumza na wajumbe wa mkutano
huoambao umefanyika katika ukumbi wa chuo cha wafanyakazi Otu jijini
Mbeya Agosti 25 mwaka huu.
Wajumbe wa
Mkutano huo wakifatilia kwa umakini hotuba za viongozi wao kabla ya
kuingia katika uchaguzi wa kuwachagua viongoizi wapya watakao kiongoza
chama hicho kwa awamu nyingine.
Na Emanuel Madafa,Mbeya
MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Nyirembe Munasa, amesema umefika wakati viongozi ambao wamebobea kwenye masomo ya
sayansi wakajikita zaidi kwenye tafiti mbalimbali ambazo zitaiwezesha serikali
kuleta mapinduzi ya viwanda hususani kwa nchi kama Tanzania.
Amesema Sekta ya viwanda, ndio sekta pekee inayoweza
kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika Taifa
lolote Duniani.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo leo jijini Mbeya, wakati
akifungua Mkutano mkuu na uchaguzi ngazi ya Mkoa wa chama cha wafanyakazi wa
Viwanda Biashara, Taasisi za fedha na ushauri, TUICO ambao ulihudhuriwa na
wajumbe kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya.
Amesema, Taifa lolote duniani linahitaji watafiti wa
kisayansi kwenye Kampuni, Taasisi na katika Viwanda kwani ndio nguzo pekee
itakayoleta mageuzi ya kiuchumi ikiwa na kupunguza wimbi la umasikini kwa
watanzania walio wengi.
Amesema kwa nchi ilipo fikia inahitaji kuwa na viongozi bora na imara kwani
viongozi imara ndio jibu la masuala yote ya maendeleo iwe kisiasa, kiuchumi na
kijamii.
Aidha, Munasa ametaka wajumbe hao, kuchagua viongozi
watakao waletea mafanikio makubwa kwa kutumia watu wa kawaida ikiwa na uwezo wa
kuamua masuala muhimu kwa kundi
wanaloliongoza.
Hata hivyo, akitoa neno la kushukuru, mjumbe wa mkutano huo,
Charles Lindi, alimuomba kiongozi huyo kutenga muda wa kutoa elimu ya uongozi
bora kwa watumishi wa umma na sekta binafsi kwani hotuba yake aliyoitoa
imeonyesha uwezo mkubwa wa utawala bora ambao mungu amembariki.
Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Tuiko Mkoa wa Mbeya
Ndugu Daudi Mpolya amewataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii na kujituma
zaidi ili kutoa chachu kwa waajili wao kutoa motisha.
0 comments:
Post a Comment